Mbeto awapa somo muhimu Vijana EA



Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimewataka Vijana Kanda  ya Afrika Mashariki na Kati  kuzipenda,  kuzilinda na kuziiepusha nchi zao kutoziingiza  kwenye kadhia ya  mivutano na  mizozo isio na ulazima  wowote. 

Pia chama hicho kimewahimiza Vijana hao  kutofuata mkumbo wa pepo za fitna na  ushawishi wenye taaswira ya nguvu ya Ukoloni  na kuridhia kupoteza uhuru,utu na  thamani ya kujitawala.

Katibu wa Kamati  Maalum ya NEC Zanzibar,   Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo  ,Khamis Mbeto  Khamis,  ameeleza hayo  huku akiyakemea makundi ya  baadhi ya Vjana wa  EA kwa  kutojali  maslahi ya  nchi zao.

Mbeto aliitaja mivutano, mabishano na   mizozio si katika njia sahihi  ya kufikia utatuzi na mapatano yanayoweza kufanyika  masahihisho kabla ya dhamira za  wachota Mali na Rasilimali za nchi  zao hawajafikia malengo  yao  .

Alisema  vyombo  vya Ulinzi na Usalama katika nchi zote   duniani ,huapa  kulinda mipaka , Usalama wa Mali na raia wake , hivyo  si vyema kwa vyombo hivyo vikachokozwa au kuvijaribiwa

" Kazi  za  Vyombo  vya dola zimetajwa  kisheria na kikatiba za nchi zote  .Hivyo si rahisi  vikakwepa kutii  dhamana hizo na   kutojilinda lilipotokea tishio la hujuma au  vurugu dhidi ya Amani ' Alisema Mbeto .

Aidha aliwaasa  Vijana   EA  kutojiona si  jukumu wenye  kuyapenda,  kuyalinda na kuyatetea Mataifa yao  dhidi ya njama zozote kwani nje ya EA ,Vijana hao hawana mahali  pa kuishi  ' Alieleza

Katibu huyo Mwenezi alisema  Waasisi wa Mataifa hayo wametumia nguvu nyingi  , kupotezwa jasho na muda wao hadi  baadhi yao  kufa kwa kupigania  Uhuru wa Mataifa hayo kwakuwa kazi ya kuleta  uhuru haikuwa nyepesi.

"Bila  Vijana kuwa na  tahadhari  watajikuta wakikwepa kubeba uzalendo  hivyo kizazi cha sasa kinaweza kuingia  katika  historia  isio na heshima . Kufuata mkumbo kama bendera  inavyofuata upepo si fahari kwao  "Alifafanua 

Vile vile , Mwenezi  huyo alisema wakoloni hawajawahi kuwa na nia njema na Afrika licha ya kurudi katika nchi zao , kwani  mara zote  huitamani  Afrika na kutaka  kuipangia masharti ya hovyo.

"Vijana wa Afrika Mashariki  na kati amkeni na  kataeni kutumiwa kwa  kuzirudisha nyuma kimaendeleo nchi zenu . Babu na bibi zenu mnaowaona leo  ni marafiki  wema kwenu hawakutaka kuondoka kirahisi  na kuiacha huru  Afrika  "Alisema Mwenezi huyo.

Post a Comment

0 Comments