Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) liko visiwani Zanzibar kunadi vivutio vyake katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara (ZITF) yalianza Desemba 29, 2026 hadi Januari 16, 2026 katika Viwanja vya Maonesho Fumba Zanzibar,
Wageni kutoka sehemu mbalimbali wameendelea kujitokeza katika banda la TANAPA kupata elimu na taarifa mbalimbali zinazohusu utalii wa ndani, uhifadhi na fursa za uwekezaji.
Maonesho haya ni fursa muhimu
kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kunadi vivutio vyake na kuhamasisha wananchi kutembelea Hifadhi za Taifa ili kufikia adhma ya serikali ya watalii milioni 8 ifikapo 2030.
0 Comments