Na Mwandishi Wetu,
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio amepokelewa katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma baada ya kuanza majukumu yake jijini Dar es salaam baada ya kupokelewa rasmi na Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Jijini Dodoa amepokelewa na Wajumbe wa Menejimenti wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Ziana Mlawa pamoja na watumishi wote wa Wizara ya Nishati, mapema leo tarehe 17 Februari, 2026.
Dkt. Mataragio anatarajiwa kuongoza timu ya Wizara ya Nishati katika kusimamia sekta ya mafuta na gesi asilia nchini, kuhakikisha usalama wa mafuta na gesi asilia pamoja na kukuza matumizi ya nishati safi na endelevu; Pia Dkt. Mataragio anatarajiwa kuchangia katika kuendeleza sekta hiyo ili kuleta maendeleo endelevu kwa taifa letu na wananchi kwa ujumla.
Pia Dkt. Mataragio ameishukuru menejimenti na watumishi wa Wizara kwa mapokezi mazuri, ameahidi kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano mzuri ili kuleta matokeo chanya katika sekta ya mafuta na gesi asilia nchini.
0 Comments