KOCHA GAMONDI RASMI KUINOA TAIFA STARS





NA MWANDISHI WETU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, ameweka wazi kuwa, Kocha Miguel Gamondi amesaini rasmi mkataba wa kuifundisha timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars).

Waziri Makonda amesema hayo wakati  akizungumza na Waandishi wa Habari  jijini Dar es Salaam, leo Februari 16, 2026, wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Kocha huyo iliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Amesema kuwa Gamondi amestahili mkataba huo baada ya kuonesha uwezo wa hali ya juu katika michuano ya AFCON 2025 iliyofanyika Morocco hivi karibuni na kuingoza  Taifa Stars kufika hatua ya 16 ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania akiwa kocha wa muda.

Serikali sasa imeamua kumwajiri rasmi ili aiongoze timu hiyo katika jitihada za kunyakua ubingwa wa AFCON 2027, ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Post a Comment

0 Comments