Na Byarugaba Innocent,Pemba
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ameridhishwa na maandalizi ya uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru,2026 yanayoendelea kwenye viwanja vya Gombani vilivyopo Wilaya ya Chakechake, Kusini Pemba.
Mhe.Abdulla amefika Kwenye viwanja hivyo leo Machi 31,2026 akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mwigulu Nchemba na kupokea taarifa inayoonesha kuwa matayarisho yote yamekamilika tayari kwa shughuli ya uzinduzi.
Aidha,Mhe.Abdulla amewapongeza Wahe.Mawaziri wenye dhamani ya Vijana Mhe.Joel Arthur Nanauka na Mhe.Shaaban Ali Othman kwa kazi nzuri ya Maandalizi hayo na kutumia fursa hiyo kuwaalika Wananchi wote kushiriki na kushuhudia tukio hilo adhimu litakalofanyika Aprili 2,2026
Mwenge wa Uhuru,2026 unakwenda na kauli mbinu isemayo "Tanzania ni yetu sote,tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo"
0 Comments