MARIAM MWINYI:ZMBF IKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA MEWATA


Mke wa Rais wa Zanzibar,  Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amekutana na uongozi wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) uliofika  Ofisini kwake Ikulu, Migombani tarehe 30 Machi 2026.

Ujumbe huo ulioongozwa na Rais wa chama hicho, Dkt. Mary Mwanyika Sando.

Aidha, Mama Mariam Mwinyi amewashukuru MEWATA kwa kuonesha dhamira yao ya kushirikiana na ZMBF katika masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya  afya,  elimu ya lishe , na tafiti mbalimbali kuhusu zao la Mwani. 

Vilevile, ameeleza kuwa ZMBF iko tayari kushirikiana na MEWATA katika nyanja mbalimbali hizo.

Naye, Rais wa MEWATA Dkt.Mary Mwanyika amempongeza Mama Mariam Mwinyi kwa mafanikio makubwa aliyoyapata kupitia Taasisi yake ya  ZMBF kwa kuwafikia Wananchi katika Kambi mbalimbali za Matibabu na uchunguzi wa afya  zilizofanyika chini ya uratibu wa ZMBF, kuwasaidia kuwainua Wanawake kiuchumi hususan Wakulima wa Mwani,  kuwasaidia Wasichana Taulo za kike aina ya Tumaini, elimu ya lishe na kuhamasisha kufanya mazoezi katika kupambana na Magonjwa yasiyoambukiza. 

Halikadhalika,  MEWATA wamemualika Mama Mariam Mwinyi kushiriki mkutano wa Madaktari Wanawake Afrika utaokaofanyika Zanzibar tarehe 05 Mei Mwaka 2027 .

Vilevile,  amefahamisha kuwa MEWATA iko tayari kushirikiana na ZMBF katika programu mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments