JUMIKITA ‘YAMFUNGIA VIOO’ MAADAM RITA KWA DHARAU ZAKE


TAARIFA KWA UMMA

Jumuia ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA) kupitia Mwenyekiti wake, Ndugu Shaaban Matwebe, imesikitishwa na kulaani vikali kitendo kisicho na heshima wala uungwana kilichofanywa na Madam Rita dhidi ya chombo cha habari cha mtandaoni.

Kitendo hicho ni kinyume na misingi ya maadili ya taaluma ya habari, na kinadhihirisha, dharau, ukosefu wa adabu pamoja na kutokujali wajibu wa kuheshimu vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla.

JUMIKITA inasisitiza kuwa taaluma ya habari inapaswa kulindwa, kuheshimiwa na kuenziwa na wadau wote bila kujali nafasi au hadhi ya mtu katika jamii.

Kutokana na tukio hilo, JUMIKITA inatoa wito kwa vyombo vyote vya habari kusitisha kumpa ushirikiano Madam Rita hadi pale atakapojitokeza hadharani kuomba radhi kwa umma pamoja na chombo cha habari kilichoathirika.

Imetolewa na:

Jumuia ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA)


Post a Comment

0 Comments