KITUO KIPYA CHA UCHENJUAJI MADINI KUJENGWA MWAKITOLYO



Dkt. Kiruswa Atoa Wito Vijana Kujitokeza Kuvitumia Kituo Cha TGC & Chuo Cha  Madini Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Madini inatarajia kujenga Kituo kipya cha Mfano cha Uchenjuaji Madini katika eneo la Mwakitolyo mkoani Shinyanga.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 15, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa wakati akijibu swali Bungeni lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mwanahamisi Athuman, aliyetaka kujua  kuhusu Mpango wa Serikali kuanzisha chuo cha madini Mkoani Shinyanga.

Dkt.Kiruswa  amesema kuwa, Serikali inatambua umuhimu wa Mkoa wa Shinyanga  katika sekta ya madini pamoja na uhitaji wa kuwajengea uwezo wananchi wake, wakiwemo vijana na wanawake katika shughuli za utafiti , uchimbaji na Uchenjuaji madini.

Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa, kwasasa Serikali inaendelea kutumia vyuo vyake katika kufundisha taaluma za madini kupitia vyuo villivyopo katika mkoa wa Dar es salaam na Tabora.

Aidha, Dkt. Kiruswa  ametoa wito kwa wananchi hususan vijana kujitokeza kunufaika na huduma na mafunzo zinazotolewa na vyuo mbalimbali vya Serikali  kikiwemo Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kilichopo mkoani Arusha na Chuo Cha Madini Dodoma (MRI) ambavyo vinafundisha taaluma za madini.

Post a Comment

0 Comments