"SERENGETI NATIONAL PARK GOLF COURSE" KETE MPYA UTALII WA MICHEZO SERENGETI





Na. Edmund Salaho - Serengeti

Uwanja mpya wa Kimataifa wa gofu unaojengwa pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti unatarajiwa kuwa miongoni mwa viwanja maarufu duniani kutokana na sifa zake za kipekee.

Akizungumza baada ya Ziara ya Waziri wa Maliasili na Utalii mara baada ya kutembelea uwanja huo ambao umeasisiwa na Bodi ya Wadhamini ya TANAPA Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Nassoro Kuji alisema Uwanja huo unakuwa mrefu kuliko viwanja vingi duniani na wa kipekee kwa kuwa wachezaji watacheza wakiwa karibu na wanyamapori.

Mhandisi Mshauri wa mradi, Dkt. Richard Matolo, Richard Matolo amesema uwanja huo utachochea utalii na kuingiza fedha nyingi za kigeni akibainisha kuwa mandhari ya wanyama wanaozunguka uwanja huo ni kivutio kisicho na mfano duniani kutokana na mazingira ya asili yanayowawezesha wachezaji kuona wanyamapori wakiwa uwanjani na kuongeza kuwa Uwanja una urefu wa kilomita 7.065,
"Pars" 72 katika mashimo 18 na kuufanya miongoni mwa viwanja virefu barani Afrika.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake za kukuza utalii nchini.

 "Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mradi huu ndani ya Serengeti kwani unaenda kuifungua Serengeti kwa kuongeza mazao mapya ya utalii wa michezo. 

"Ile dhana ya "Golf Tourism" inayokua duniani Mhe. Rais ameitekeleza kwa vitendo. Uwanja huo unatazamiwa kuwa alama mpya ya utalii na michezo Tanzania"

Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mhe.Angelina Marco Lubela amemshukuru Rais Samia kwa kuleta fedha za kutekeleza mradi huu katika wilaya Serengeti na kuahidi kuulinda uwanja huo kwa wivu mkubwa kwani ni fursa kwa vijana wetu ni fursa ya ajira.

Uwanja una urefu wa kilomita 7.065 na "Pars" 72 katika mashimo 18 miongoni mwa viwanja virefu barani Afrika.

Post a Comment

0 Comments