Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wananchi kutambua, Mwenge wa Uhuru ni miradi ya maendeleo hivyo chama hicho hakitawavumilia watendaji wa serikali ambao Mwenge umepita katika maeneo yao na kubaini ubadhirifu katika miradi ya wananchi.
Akizungumza Mjini, Unguja leo 01 Aprili 2026, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo, Komredi Khamis Mbeto Khamis alisema itakapobainika watazishauri mamlaka zingine hatua za kuchukua zikiwemo za kisheria.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Mwenge kuwashwa kesho 02 Aprili 2026 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Uwanja wa Gombani Mpya, Mkoa wa Kusini Pemba.
Mbeto alisema watafanya hivyo ili liwe somo yeyote aliyepewa dhamana ajue anafuatiliwa na sisi ndio mtaji wetu kupeleka huduma bora kwa wananchi ili watuamini tena na kutuchagua tana 2030.
Mbeto alisema Mwenge unapopita mara baada ya kuwashwa unaenda kukagua utekelezaji wa miradi na ilipofikia na kuishauri wizara ili kukamilisha palipobakia, unapozimwa.
“Ni vema wananchi wakajua serikali
inapeleka pesa nyingi kwenya miradi na ripoti zifanyiwe kazi na sisi kama CCM
hatutakubali tutahakikisha maelekezo ya Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM
Taifa, yanafanyiwa kazi” alisema Komredi Mbeto.
Alibainisha kuwa mathalani serikali
imeelekeza vijengwe vituo vya afya 120 nchi nzima, visipotengenezwa anayekuja
kuadhibiwa ni CCM hiyo maana yake nini? CCM ndio inaenda kwa wananchi kuomba
kura sio serikali” alisema.
Mwenezi huyo alieleza kuwa kama mtu kakabidhiwa fedha kujenga zahanati, shule, kupeleka maji fedha anaziharibu, ripoti inakuja kama hiyo ya Mkaguzio Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CCM haitakubali.
“Tutaendelea kusimamia serikali na kuhakikisha waliosababisha mapungufu yote wana wajibika lengo wananchi wapate huduma bora na ikifika 2030 waendelee kuichagua CCM” alisema Mbeto.
Mbeto aliunga mkono kauli mbiu ya
Mwenge wa Uhuru Mwaka huu isemayo ‘Tanzania ni yetu sote tushirikiane kuleta
maendeleo’ na kusema kuwa nchi sio ya Rais Dkt. Samia au Rais wa Zanzi.

0 Comments