MBETO: DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI ISILIPASUE TAIFA LETU


Na Mwansishi Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimeviasa Vyama vya Upinzani na kuvitaka vielewe maana ya  demokrasia ya Vyama Vingi si kuizuia Serikali isitimize wajibu wake au ihofie kuchukua hatua za Kisheria pale itakapobidi.

Kadhalika CCM kimeutaja ushindani wa Kisiasa ikitaka uwe ni mchuano wa hoja  na sera, si kukithiri matusi au kupandikiza  hasama na chuki.

Hayo yametamkwa  na Katibu wa Kamati Maalum  ya NEC  Zanzibar,  Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo , Khamis Mbeto Khamis  Visiwani  humu.

Mbeto yuko katika Msafara wa   Makamu Mwenyekiti  wa CCM Zanzibar ,Rais Dk Hussein Ali Mwinyi ,ziara  inayoendelea katika  Mkoa wa Kaskazini Unguja .

Akizungumza kwa  masikitiko alisema inashangaza kwa baadhi ya Viongozi wa Upinzani  , wakisikika katika hotuba  zao zikihamasisha hasama kwa lengo la  kulipasua au  kuligawa Taifa 

"Ushindani wa Siasa za chuki, hasama na matusi si kielelezo cha ustaarabu wa  kisiasa . Tunawaonya wenzetu waache Siasa zisizo na  manufaa kwao , kwetu na kwa jamii  yetu " Alisema Mbeto 

Pia Katibu  Mwenezi  huyo alisema  tabia ya  baadhi ya Wanasiasa kutoa vitisho au madai  yasio na ushahidi , hakuthibitishi kupevuka kwao badala yake  Wananchi huwapuuza .

"Huwezi  kubagaza Utu  na heshima ya  wenzako kisha uachwe  ukitamba Mitaani. Vyombo vya dola na vya  Kisheria vipo makini. Kutuhumu wenzako  kwa masuala yasio na   ushahidi si uungwana  "Alieleza

Mbeto  alisema  Siasa ni ushindani wa kimantiki unaoshindanisha  hoja na  sera. Tunaelewa  kazi ya upinzani ni kufichua uovu ndani ya utawala lakini kuwe na  ushahidi  na vielelezo  si kutamka matusi  mbele  ya jamii.


"CCM haijawahi kuhofia  upinzani toka mwaka 1992.   Walikuwepo kina  Mabere Marando , Chifu  Fundikira, Mapalala, Maalim Seif , Kambona  ma Mloo walikuwa hawakutoa matusi .Walitoa hoja na kujibiwa kwa nguvu ya  hoja " Alifahamisha 

Aliwataja  Viongozi hao huku  akisifu kuwa walikuwa  wamekomaa  na wajenzi wa   hoja makini na waliojua  umuhimu wa   Amani na Umoja  bila kutoa vitisho au kueneza  chuki za kisiasa.akizungumzia kauli ya makamu mwenyekiti wa ccm na Rais  wa zanzibar  kuhusu serekali  ya umoja wa kitaifa na mazungumzo ya kusaka muwafaka,

mbeto  amesema kauli ya makamu mwenyekiti  na Rais  wazanzibar  ipo wazi na ndio msimamo wa ccm

mbeto  aliengeza kwamba tutazungumza kwa  yale mambo yanayo husiana na sheria ya serekali  ya umoja wa kitaifa kama kutakuwa na mambo ambayo hayapo kwenye  yale mambo yaliyo wekwa kwenye  sheria, 

hayo yatahitaji maamuzi ya vyombo  husika kama baraza la wawakilishi  na vyombo vyengine vinavyo husika vilivyo wekwa na katiba ya zanzibar  na sheria zake, huwezi kutaka mambo ambayo kwa mujibu wakatiba yapo kwenye mamlaka ya Rais, akimalizia mwenezi  mbeto.

Post a Comment

0 Comments