UJIO WA KAGAME, RUTTO AIBU KWA MAKUWADI WA KISIASA EA-MBETO



Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimetaja ziara za Marais wa Rwanda na Kenya  nchini ni majibu tosha kwa   Wanasiasa na Wanaharakati  uchwara,  wanaojihusisha na   Ukuwadi wa Kisiasa Afrika Mashariki.

Hivyo  basi,  CCM kimewataka  Wana Afrika Mashariki wote kupuuza  uvumi  usio na mashiko ukidai Mataifa  EA  hayana Uhusiano Mwema . 

Matamshi  hayo yametamkwa na Katibu  wa Kamati  Maalum ya  NEC  Zanzibar, Idara ya Itikadi , Uenezi  na Mafunzo , Khamis  Mbeto Khamis ofisini kwake kisiwandui Visiwani Zanzibar.

Mbeto alieleza hayo mara baada ya Marais hao kuitembelea   nchi huku akieleza kuwa  Uhusiano wa Tanzania kidiplomasia  wa Kikanda na Kimataifa ,hautadhoofika 

Mbeto alisema  wapo baadhi ya  Wanasiasa na Wanaharakati Uchwara EA ambao   uelewa wao ni hafifu katika Uongozi ,Siasa na  Utawala  , hueneza taarifa hasi zikidai Tanzania haina Uhusiano mzuri na Nchi jirani. 

Alisema Tanzania itaendelea kufuata   kanuni , taratibu ,  misingi ya  Uongozi ,Utawala wa Sheria bila kukiuka  kanuni za  kidiplomasia   ,na kwamba  itaheshimu  miiko na kanuni ili kudumisha Umoja  na Ushirikiano. 

"Wako wapi  Wanasiasa na Wanaharakati viherehere  wakaanga sumu,   chuki na uongo . Ziara za Marais Poul Kagame na  Dk William Rutto zimewatia aibu  Makuwadi  wa kisiasa na wapika  Majungu EA " Alisema Mbeto .

Aidha, Katibu huyo Mwenezi ,  alisema Tanzania na jirani zake , Washirika  wa Maendeleo, Wawekezaji, Jumuiya ya   EAC   ,Jumuiya za kikanda na  Mashirika ya Kimataifa , itaendeleza  Ushirikiano usio na  shaka . 

"Mataifa  yetu yatizame  mbele na  kuanzisha Miradi  ya Kiuchumi itakayotanua wigo  wa Ajira na  Uwekezaji . Tungependa kuziona  Sekta za  Mawasiliano, Usafiri na Biashara  zikiimarika  .Tanzania daima  haitatikiswa na kelele  za Wakaanga Sumu " Alieleza. 

Pia Mbeto  alisema kwa miaka  mingi Tanzania  imekuwa ikifanyakazi   kwa Ushirikiano na Nchi zote jirani , hivyo uchonganishi  wenye  lengo la kuchochea  mitafaruku,  idhibitiwe mapema  kwa nguvu  ya pamoja. 

"Tusingoje hadi  hatari  ishamiri  ndipo udhibiti ufanyike . Tulinde mipaka yetu kwa nguvu na sauti  moja. Uchonganishi na Uchochezi udhibitiwe ili usidhoofishe   Umoja , Amani  na Maendeleo  " Alisisitiza Mbeto.

Mwenezi huyo  akizungumzia nafasi ya  demokrasia, Uwazi na Utawalabora , alisema   Wananchi wamepewa uwanja mpana wa ushiriki wa  demokrasia inayozingatia  nidhamu, miiko  na utii wa sheria.

'Serikali  zimetoa nafasi pana ya Utekelezaji wa  demokrasia shirikishi  na si  demokrasia  holela.  Serikali zetu zinaheshimu  sheria ,  Uhuru wa Kijamii wenye mipaka kwa mujibu wa sheria na katiba "   Alisema Mbeto

Post a Comment

0 Comments