Mbeto:Ni kosa kudhani Demokrasia maana yake hadi CCM ishindwe



Na Mwandishi  Wetu,Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimesema ikiwa tafsiri  na maana   ya  Demokrasia kwa Upinzani ni kuona  CCM  ikishindwa Uchaguzi , kupoteza  Viti vya Udiwani, Ubunge na Uwakilishi , hiyo si tafsiri wala    mantiki sahihi ya neno Demokrasia .

Aidha CCM kimeapa  hakiwezi kushindwa  na  Vyama vilivyoundwa kuanzia Mwaka 1992, kwa kudhani  tayari viwe na  nguvu  za  kukishinda chama kilichoshika Madaraka  Miaka zaidi ya Sitini .

Matamshi hayo yametamkwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar, Idara ya Itikadi,  Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto  Khamis , alipozumgumza na Waandishi wa Habari ofisini  kwake  Kisiwandui  Kisiwani Unguja. 

Mbeto alisema  nguvu za chama chochote cha siasa duniani,  ni  umri na uimara wa chama hicho  , Rasilimali  Watu na Fedha, Mitaji na Vitega  Uchumi,  Sera makini ,   Oganaizesheni  ilioshamiri na mtandao madhubuti wa kisiasa

Alisema CCM  ni chama kilichojijenga kimtandao kipo kila kona Tanzania ,kina Rasilimali  Watu, Mitaji na Vitega Uchumi,  hivyo si jambo rahisi kudondoshwa  na  Vyama viliundwa Mwaka 1992.

"Ni ajabu kusikia Upinzani  ukidai kura zake zinaibiwa. Vyama hivyo bado vichanga Kisiasa  havina ubavu wa kushindana na CCM.  Hata timu changa za Soka hazihimili  mikiki mikiki dhidi ya Simba au  Yanga Uwanjani " Alisema Mbeto 

Aidha  akisema bila kukitaja jina  chama kimoja  cha upinzani, alidai kimeweza kununua jengo jipya la Ofisi  zake baada ya  kulipwa ruzuku  kutoka katika Serikali  za CCM ,huku chama hicho kikijigamba  kina  uwezo wa   kuidondosha CCM .

Alipoulizwa iwapo Serikali za CCM  zipo tayari kufanya  mabadiliko ya katiba ,mifumo ya Uchaguzi, kitaasisi na  sheria ya  Uchaguzi , Mbeto alijibu kipo tayari ingawaje kusitokane na  shindikizo au kwa vitisho 

"Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameahidi  kabla hajaondoka madarakani mwaka 2030  Tanzania itapata Katiba mpya. Lakini hata ikipatikana Katiba  , mabadaliko ya mifumo na sheria ,  upinzani  haujapata na uwezo wa kuishinda CCM" Alieleza 

Katibu  huyo Mwenezi  alisema ikiwa neno  Demokrasia  kwa tafsiri  ya Upinzani    hadi  pale  kishindwe uchaguzi , vyama hivyo vitasubiri  kwa miaka mingi kwakuwa CCM bado kitaendelea kuungwa mkono wananchi na kuongoza  dola. 

"Nimemsikia Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo  Othman Masuoud Othmam akidai CCM kimejiweka madarakani. Muulizeni kimejiweka kivipi .Je Uchaguzi haukuafanyika  .Vyama havikushriki Uchaguzi na  je Tume ya Uchaguzi huikumtangaza mshindi ?, " Alihoji  Mwenezi huyo.

Mbeto alimtaja  Mgombea  huyo wa  Urais  Zanzibar  kupitia  ACT Wazalendo, hajawa na  sifa za kumshinda Mgombea Urais wa CCM Rais  Dk Hussein  Ali Mwinyi ,cha ajabu amekuwa akisimama na kudai  ameibiwa kura .

"Ni kura zipi  hizo alizoibiwa Othman. Yeye alikuwa wapi  wakati kura zikiibiwa .Ziko wapi  na kwanini hakuwakamata walioiba. Kama kuiba Kura  jambo  rahisi yeye  na chama chake walishindwaje kuiba! "Alishangaa.

Hata hivyo Mwenezi  huyo alisema kwa nafasi ya Urais  Zanzibar, alimtaja  Othman kuwa. Mwanasiasa mpya  asiye na   umaarufu ndani na nje ya    ACT  ,  kwa asili na historia  ya Siasa  za Zanzibar,  si mtu anayetambulika na kukubalika.

Post a Comment

0 Comments