Na Victor Masangu,Pwani
Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani imeamua kuwajengea uwezo na maharifa madiwani wote wa viti maalumu kwa kuwapatia semina elezeki ambayo itawasaidia katika kutekeleza majukumu yao.
Katika semina hiyo ambayo pia imehudhuliwa na makatibu wa UWT ngazi za Wilaya imelenga kuwajengea uwezo ikiwa pamoja na kuwakumbusha wajibu na majukumu yao ya kila siku ya ndani ya chama na jumuiya.
Katibu wa jumuiya ya wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani Aziza Hussein amebainisha kwamba katika semina hiyo madiwani wamekumbushwa katika suala la kusimamia miradi ya maendeleo.
Pia katibu huyo amesema kwamba madiwani hao wameweza kupatiwa mbinu mbali ambazo zitaweza kuwasaidia katika kutatua changamoto ambazo zinawakabili wananchi.
"Tumeandaa semina hii ya kuwakutaniisha madiwani wote wa viti maalumu kutoka Mkoa wetu wa Pwani na lengo kubwa ni kuwajengea uwezo wa kutatua mambo mbali mbali ambayo wamekuwa wakiyatekeleza katika maeneo yao,"amebainisha katibu huyo.
Kadhali amesema kwamba semina hiyo imewapa fursa ya kujifunza umuhmu wa uwepo na bima ya afya kwa wote na namna bora ya kutambua kazi zao ikiwa pamoja na kupendana na kuwa na umoja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu amebainishs kwamba semina hiyo itakwenda kuwa msaada mkubwa kwa madiwani hao wa viti maalumu.
Mwenyekiti huyo amesema kwamba kwa sasa madiwani hao wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano katika kuimarisha uhai wa chama pamoja na jumuiya ya wanawake wa UWT Mkoa wa Pwani.
Nao baadhi ya madiwani wa viti maalumu akiwemo Tatu Mpeki kutoka Wilaya ya Mkuranga amesema semina hiyo waliyoipata itakuwa ni chachu kubwa na kwamba ameahidi kuyafanyia kazi yale yote ambayo wamefundishwa.
Pia ameupongeza uongozi wa UWT Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuona umuhimu mkubwa wa kuwashirikisha madiwani wa viti maalumu ambao wameweza kupata elimu ambayo watakwenda kuifanyia kazi kwa maslahi ya chama na jumuiya.
"Tunashukuru sana kwa dhati kwa uongozi wa UWT ngazi ya Mkoa kwa kuona umuhimu wa kutukutanisha kwa pamoja na kutupa semin hii ambayo kwetu ni hatua muhimu sana kwa sisi madiwani wa viti maalumu na kwamba tutayafanyia kazi yale yote ambayo tumefundishwa,"amesema Mhe.Tatu.
Semina ya madiwani wa viti maalumu Mkoa wa Pwani imeandaliwa na uongozi wa Jumuiya wa wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwapa mbinu mbali mbali ambazo zitawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya chama na jumuiya.


0 Comments