WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AKUTANA NA UJUMBE WA JESHI LA JAMHURI YA ALGERIA


NA MWANDISHI WETU

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, (Mb) tarehe 11  Mei 2026 katika ofisi ndogo za Wizara,Upanga jijini Dar-es-salaaam, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Jeshi la Algeria ukiongozwa na Brigedia Jenerali Abbas Ibrahim.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria katika masuala ya ulinzi na usalama pamoja na mafunzo ya kijeshi. Katika mazungumzo hayo, Brigedia Jenerali Abdala alitumia fursa hiyo kumfikishia Dkt. Nyansaho salamu kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Algeria na Rais wa Jamhuri ya Algeria, Mheshimiwa Abdelmadjid Tebboune, ambaye ameipongeza serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza amani na utulivu na kuifanya Tanzania kuwa kisiwa cha amani. Aidha, Brigedia Jenerali Abbas Ibrahim  amemueleza Dkt Rhimo Nyansaho kuwa nchi ya Algeria inajivunia mahusiano ya muda mrefu na kihistoria kati ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo kati ya Waziri wa Ulinzi na JKT na Ujumbe wa Jeshi la Jamhuri ya Algeria yalihudhuriwa pia na Balozi wa Algeria nchini Tanzania na maafisa waandamizi toka Wizara ya Ulinzi na JKT na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
https://youtu.be/kDj8AcMeuH8?si=cYLHrObxtKTfP6Rc

Post a Comment

0 Comments