*Ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali-Mtumba Wafikia 95%
Mwanza
Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini kwa kupunguza barabara za changarawe na kujenga barabara za lami katika wilaya mbalimbali, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kuinuka kiuchumi kupitia shughuli za usafirishaji.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alipokuwa akizungumza na Maofisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) unaoendelea jijini Mwanza.
Msigwa amesema maofisa Mawasiliano wanapaswa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwa kuwa miradi hiyo ni ya manufaa kwa wananchi wenyewe.
“Sisi ndiyo tunaobeba taswira ya Serikali. Tunapaswa kuwaonesha wananchi fursa zilizopo kutokana na uwekezaji mkubwa

0 Comments