■ Waziri Mavunde ataka mnyororo wote wa utoroshaji wa madini hayo udhibitiwe,
■ Asikitishwa na upotevu wa mapato ya Serikali yatokanayo na vitendo hivyo,
■ Aelekeza wahusika wote wafutiwe leseni na kutoruhusiwa tena kufanya biashara ya madini,
■ Atoa rai kwa wananchi kufanya biashara ya madini kupitia mfumo rasmi
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,
Kufuatia kuimarishwa kwa mfumo wa udhibiti wa biashara haramu ya madini unaofanywa na Wizara ya Madini kupitia Kikosi Kazi (Taskforce), madini aina ya dhahabu Gramu 4,402.20 yenye thamani ya
1,238,458,594.42 yamekatwa yakitoroshwa.
Hayo yamesemwa leo tarehe 27 Julai, 2026 na Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb) Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari.
"Serikali kupitia Wizara ya Madini iliunda Kikosi kazi ambacho kinahusisha vyombo vya dola ili kudhibiti biashara haramu ya madini na utoroshaji. Hii ni sehemu tu ya kazi ambazo zimeendelea kufanywa na Kikosi kazi hicho katika kuimarisha mfumo wa ufanyaji biashara ya madini"
"Ndugu zangu, dhahabu hii yenye zaidi ya thamani ya bilioni 1.2 haikupitia katika mfumo rasmi wa ufanyaji biashara ya madini na hivyo kupelekea Serikali kukosa mapato ambayo yangeisaidia kuimarisha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi" Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa dhahabu hiyo iliyokamatwa imetaifishwa kwa mujibu wa taratibu za Sheria na imehifadhiwa Benki Kuu ya Tanzania.
Vilevile, Mheshimiwa Mavunde amekielekeza Kikosi Kazi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kumhoji vizuri mtuhumiwa aliyekamatwa na dhahabu hizo kufahamu alikotoka na alikuwa anapeleka wapi, ili kuweza kutibu kabisa mzizi wa vitendo hivyo na kuvunja mnyororo wa wote wa utoroshaji.
Mhe. Mavunde alisisitiza kuwa, iwapo mtuhumiwa aliyekamatwa alikuwa na leseni ya ufanyaji biashara ya madini kufutiwa leseni hiyo mara moja na kuingizwa kwenye orodha maalum ya wenye makosa (blacklisted) ili asiruhusiwe tena kufanya biashara ya madini nchini.
Katika hatua nyingine, Waziri Mavunde alitoa rai kwa wananchi wote kuzingatia na kufuata sheria na mifumo ya ufanyaji biashara ya madini ambayo tumejiwekea kupitia masoko ya madini na vituo vya ununuzi ambavyo vimesambaa Nchi nzima.
.jpeg)
.jpeg)

0 Comments