MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BAOBAB YALETA NEEMA KWA KUKUSANYA FEDHA KUSAIDIA WATOTO YATIMA


Na Victor Masangu, Bagamoyo  

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu  Ndemanga amewahimiza viongozi na wananchi mbali mbali wakiwemo  wadau, wanafunzi, walimu,kuhakikisha wanajenga tabia ya kushiriki kikamilifu katika  michezo mbali mbali kwa lengo la kuweza kujenga afya zao  ikiwa pamoja  na kuondokana  kabisa na  changamoto ya kuwa na magonjwa yasiyoambukiza.

Hayo ameyabainisha wakati  wa ufunguzi rasmi wa  sherehe za maadhimisho  ya miaka 20 ya   Baobab  tangu kuzaliwa kwake  ambayo yameweza kushirikisha jumla ya washiriki zaidi ya ya elfu 1000  kutoka maeneo mbali mbali wakiwemo wadau wa michezo, wanafunzi, taasisis wezeshe pamoja na  viongozi mbali mbali wa serikali.
 ,
Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kuwa kwa sasa jamii inapaswa kubadilika na kujikita zaidfi katika kufanya mazoezi ambayo yataweza kuwasaidia katika kujenga afya zao na kuondokana kabisa na magonjwa hivyo   amewahimiza  wananchi  wa Wilaya ya Bagamoyo  na maeneo mengine  kuendelea kujitokeza kwa wingi pindi inapojitokeza michezo mbali mbali kama vile mbio za Marathon na michezo mingine.

"Niwapongeze kwa dhjati uongozi wa Baobab kw akuweza kunialika katika sherehe hizi za maadhimisho ya miaka 20 na mimi kama mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  nimewza kushiriki kikamilifu katika mbio za Marathon kwa hiyo kitu kikubwa ninachowaomba  wananchi ni kuwa na tabia ya kushiriki katika michezo ili kuondokana na magonjwa mbali mbali,"amebainisha Mkuu huyo.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Taasisi za Shajar Shani Swai ambaye   ndio  inayoimiliki shule ya Sekondari Baobab  amebainisha kwamba  lengo kubwa katika  Marathon hiyo ni kukusanya fedha  kiasi cha  zaidi ya shilingi  milioni 20  kwa lengo la  kuweza  kuwasaidia watoto wenye ulemavu na wanaoishi katika mazingira magumu.

"Tunashukuru sisi kama taasisi tumeweza kutimiza miaka 2o tangu kuanzishwa kwake na mimi napenda kusema lengo kubwa ya kufanya marathon hii ni kukusanya zaidi ya milioni 20 ambayo itaweza kusaidia katika kusaidia watoto yatima na wale amabo wanaoishi katika mazingira magumu na  tunashukuru tueweza kutimiza malengo yetu,"amebainisha mkurugenzi.

Naye  Mwanzilishi wa Taasisi  hiyo ya Shajar  Sophia Swai amebainisha kwamba wamemua  kutumia  maadjimisho hayo ya miaka 20  kukusanya fedha hizo ambazo zitaweza kuwasaidia watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu pamoja na jamii mbali mbali ambazo zinauhitaji.

Katika maadhimisho hayo ya miaka 20  ya  Baobab kumefanyika   mbio za kuanzia kilometa 5 hadi kilometa 10 ambapo  michezo mbali mbali imefanyika ikiwemo, soka,kikapu, pete,Riadha, kuvuta kamba ambapo washindi wameweza kuzawadiwa zawadi mbali mbali ya vikombe pamoja na medani.

Post a Comment

0 Comments