MAPOKEZI NAIBU KATIBU MKUU CCM YAZIDISHA MATUMAINI PEMBA.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama cha  Mapinduzi kimesema  msingi wa kukubalika kwake na Wananchi si umaarufu wa jina lake,  bali ni kutokana na  Mikakati  ya Utekelezaji wa Sera zake unaomvutia  kila Mtanzania .

Aidha, CCM kimeahidi kuendelea kutumikia Wananchi kwa sababu hakuna chama cha Siasa sahihi  nchini chenye uwezo , upeo na  sifa za CCM.

Matamshi  hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itkadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamisi, mara tu  alipowasili  Kisiwani Unguja akitokea  Pemba.

Mbeto alisema Wananchi wa Tanzania  kwa ujumla wao , bado wana imani kubwa kwa  CCM,  kutokana na uimara wa Sera zake ambazo kwa miaka yote zimesimamia Amani, Umoja na Maendeleo.

Alisema wakiwa Kisiwani Pemba, Wananchi na Wanachama wa CCM  wamejitokeza kwa mamia  kumlaki Naibu Katibu  mkuu  mpya, Abdi Mahmoud Abdi kisiwani humo.

"Ziara yetu  Kisiwani Pemba imekuwa na mafanikio makubwa. Kujitokeza kwa wingi  Wananchi katika mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wetu  ni ishara ya Uhai wa chama chetu ndani ya umma" Alisema Mbeto.

Vile vile, Katibu huyo Mwenezi  alisema kujitokeza  huko kwa wingi kwa wananchi na  mapokezi yaliotikisa  ,si ishara peke yake ya kuungwa kwake mkono kwa CCM, bali ni mwanzo wa maandalizi  kuelekea Mwaka 2030.

"Mila na desturi  ya CCM unapomalizika Uchaguzi Mkuu mmoja huwa  mwanzo wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao. Tumeanza kujiandaa kuelekea kupata ushindi ujao. Ushindi wetu hutokana na nguvu ya Umma" Alieza.

Mbeto alisema ni makosa kwa chama cha Siasa  makini kuanza kujiandaa ili kupata ushindi wa  uchaguzi ujao,  katika mwaka huo huo wa Uchaguzi. CCM  hivyo ndivyo kinavyoishi Kisiasa" Alifafanua . 

Hata hivyo , Mwenezi huyo alipoulizwa anaitazama vipi  nafasi ya Wapinzani wao Kisiasa Visiwani Zanzibar, alijibu akisema  inashangaza wenzao kuamua kuwa wapinga maendeleo huku CCM ikiendelea kupigania Maendeleo.

"Kupiga domo la  Siasa kila uchao mabarazani bila msukumo wa  Maendeleo ni kama kucheza kamari. Wananchi wanahitaji  maisha bora, kuimarika kwa huduma za jamii na Uchumi mwanana "Alisisitiza .

Mbeto alisema  nia ya CCM ni kufanyakazi na wenzao wa ACT Wazalendo katika Serikali ya Umoja  wa kitaifa pia kushirikiana na vyama vingine vya Siasa katika nyakati zote.

Post a Comment

0 Comments