Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kimetaja msingi wa  Tamasha la Kizimkazi  Mkoa wa Kusini Unguja, umebeba maudhui ya kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni,Mila na Desturi za watu wa  Zanzibar.

Aidha,Tamasha hilo hukusudia kuanzisha ,kuendeleza na kuibua miradi ya kiuchumi na kimaendeleo katika jamii.

Hayo yameelezwa na Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto khamis, alipozungumza na Waandishi wa habari waliofika ofisini kwake Kisiwandui.

Mbeto alisemaTamasha hilo halina sura ya  Kisiasa bali limejielekeza   kuonesha ustaarabu, Mila,Utamadumi ,silka  akhlaq, michezo na shughuli za watu Mkoa Kusini Unguja .

Alisema kila jamii hutofautiana kwa tabia  zao , kazi za Uzalishajimali, Kiuchumi na kijamii ,zikiwemo  ngoma,unyago,jando, harusi na mikusanyiko ya Jadi na Asili za watu wake.

"Kuna mikusanyiko isiopishana sana kwa Mila ,Utamaduni, ustaarab,  ngoma za Asili, lahaja na matamshi ya Lugha ya Kiswahili baina ya Mkoa  hadi Kisiwa kimoja na  kingine" Alisema Mbeto.

Aidha, alisema ndani kiini cha Tamasha hilo, Tamasha  huonesha aina ya mapishi ya Mkoa wa  Kusini Unguja, shughuli jumuishi za Uzalishajimali, Sanaa,Ufundi stadi , kazi za mikono na maeneo ya Kihistoria.

"Kuna  hadithi  na simulizi za  kihistoria kwa wenyeji na wageni  wahamiaji wa Kale  waliofika na kuishi Kizimkazi.Hadithi hizo hutofautiana na zile zilizoko kisiwa cha Unguja,  Tumbatu na Pemba "Alieleza.

Katibu huyo Mwenezi  alisema hata mapokeo ya harakati za  Kisiasa pia kuna mitazamo na ushiriki wake ,kwakuwa Siasa haitenganishwi na  maisha ya jamii,  juhudi  na harakati za  kujikomboa kwao .

"Tamasha la Kizimkazi la  kila mwaka huwaunganisha wana jamii  na kuwaweka pamoja. Mikusanyiko hiyo huhimiza Umoja ,Ushirikiano , Upendo na Udugu Alisistiza

"Hatua ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kupita mitaani ndani ya Hifadhi ya Mji Mkongwe . Akisalimiana na wenyeji na watalii ni katika kuhimiza Umoja na upendo . Dunia ya leo inahitaji maelewano si migawanyiko"Alieleza Mwenezi  huyo.