MBETO: UTEKELEZAJI MIRADI YA KIMKAKATI WAMPA HESHIMA RAIS DKT. SAMIA KIMATAIFA

Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar

Chama cha Mapinduzi kimempongeza  Rais  Dk Samia Suluhu  Hassan kwa utekelezaji miradi ya kimkakati , ushawishi wake kimataifa , kuaminika kwake  ,sanjari na   uamuzi wa  Wanahisa wa Taasisi ya Africa50  na Jukwaa la Miundombinu Afrika,  kufanya mkutano wake  Tanzania.

Kadhalika CCM kimeutaja uwezo wa  Rais Dkt Samia Kimataifa,ushawishi , kuaminika kwake, ni ishara  ya utendaji makini wa Serikali yake  ukiungwa mkono  na Taasisi  za Kimataifa.

Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo , Khamis Mbeto Khamis ,aliyesema Serikali ya Dkt Samia  kutokana na  juhudi za usimamizi thabit  wa wa  kisera, Serikali  yake ikifikia malengo na shabaha za  Kimataifa.

Mbeto alisema  Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu, aghalabu  huharakisha  utekelezaji wa miradi yenye ubora ya miundombinu,  kupitia uwekezaji wa pamoja na kuongeza thamani ya fedha.

Aidha alisema kutokana na utekelezaji wa  mikakati  ya kisera ,  Serikali ya Tanzania  imekuwa ikivutia zaidi kutokana na  kushirikisha  mitaji ya sekta binafsi inayoimarisha Maendeleo ya kiuchumi Barani Afrika.

"Mkakati wa Kuharakisha Ujenzi wa  Miundombinu na kukamilisha miradi ya kimkakati kwa  viwango .Kwa  muktadha huo juhudi hizo na nyingine zinaibeba Tanzania mbele ya Mataifa mengine Afrika "Alisema Mbeto.

Pia Katibu huyo  Mwenezi alisema hatua ya Serikali ya Rais  Dkt Samia , ikiwemo hatua  ya kuvutia Wawekezaji ,  kuzishirikisha sekta binafsi na ya umma kwenye uwekezaji wa Nishati, Usafirishaji, na gesi Asilia , kunaipa heshima ya juu Tanzania.

"Baadhi ya wenzetu kwa kulazimisha umaarufu wa kisiasa  hupotosha hata maendeleo yanayoonekana kwa macho. Ni kinyume  na Tanzania inayotazamwa  Kimataifa. Kupanda kwa thamani na matumizi ya  rasilimali   gesi na kumeimarisha Viwanda na Ajira"Alisema Mbeto .

Katibu huyo Mwenezi alisema si hivyo  tu, lakini pia kuonyesha Usalama wa Uwekezaji, kunafikisha ujumbe duniani  kuwa Afrika ni eneo salama la kimkakati linaloshamirisha  maendeleo kwa kasi.

Viongozi mbalimbali toka Mataifa ya Afrika wanahudhuria Mkutano katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo pia unahudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ya miundombinu, huku mgeni rasmi akiwa  mwemyeji wake Rais  Dkt Samia .

Post a Comment

0 Comments