MWENYEKITI UWT KIBAHA MJI ATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI WANAWAKE KATA YA MSANGANI NA MKUZA




Na Victor Masangu, Kibaha
 
Katika kupambana na wimbi la umasikini na kuachana na kuwa tegemezi kwa wanawake Mwenyekiti wa  Jumuiya ya wanawake  (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja  ameamua kutoa  darasa maalumu  kwa ajili ya kufundisha  mafunzo ya ujasiriamali na jinsi ya kutenghheneza bidhaa   kwa  wanawake  mbali mbali  kwa lengo la kuweza kuwasaidia kuachana na kuwa tegemezi ikiwa sambamba na  kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamebaishwa  wakati wa ziara yake maalumu yenye lengo la kuweza kukutana na baadhi ya makundi ya wanawake kwa ajili ya  kutoa darasa la mafunzo mbali mbali ya ujasiliamali yenye lengo la kuwaongozea ujuzi na  elimu ambayo itawasaidia katika kutengeneza biadha za aina tofauti.

Mwenyekiti huyo  ametoa darasa la mafunzo hayo kwa wanawake wa jumuiya ya UWT katika kata mbili za Msangani  na Kata ya  Mkuza ambapo zaidi ya wanawake 100  wameweza kupatiwa mafunzo mbali mbali ya kutengeneza bidhaa mbali mbali ikiwemo kufundisha jinsi ya kutengeneza  bidhaa za batiki, sabuni za kuogea, sabuni za chooni,shampuu kwa ajili ya nywele.

 Mgonja  amebainisha kwamba  ametoa  kutoa elimu hiyo ya darasa la  mafunzo ya ujasiriamali bure bila malipo ikiwa ni utekelezaji wake wa ahadi ambayo aliitoa wakati akiwa katika ziara yake ya kuwashukuru wanawake hao ambao waliweza kukiheshimisha chama wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambapo waliweza kupiga kura za kisdindo.
"Ahadi ni deni kwa hiyo mimi kama Mwenyekiti wa UWT nimekuja kuwapa elimu na mafunzo mbali mbali ya ujasiliamali bila malipo ya iana yoyote na kwamba mafunzo hayo ni moja ya ahadi yangu  ambayo niliitoa wakati nikiwa katika ziara yangu ya kutoa shukrani kwa wanawake  kukipigia chama cha mapinduzi kura nyingi za kishindo katika uchaguzi mkuu,"amebainisha Mwenyekiti Mgonja.
 
Kwa upande wake Katibu katibu wa UWT  Cesilia Ndaru amewahimiza wanawake kuhakikisha kwamba wanatumia fursa mbali mbali  za ujasiriamali na kuachana kabisa na tabia ya kuwa na majungu na  kuzungumza maneno ambayo hayana faida yoyote na badala yake wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali.

Naye  mjumbe wa kamati ya utekeelzaji wa UWT Zainabu Gama amebainisha kwamba  darasa la mafunzo hayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wanawake hao katika kujiongezea kipato  na kujikwamu kiuchumi.

Nao baadhi ya wanawake kutoka kata za Msangani na Mkuza ambao wameweza kupata fursa ya kupata elimu hiyo  ya kutengeneza bidhaa mbali mbali wamesema  wamempongeza Mwenyekiti wa UWT kwa kuwapatia darasa hilo la elimu  ambayo itakwenda kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua na  wimbi la umasikini na kujikwamua kiuchumi.

Ziara  maalumu ya  Mwenyekiti wa UWT Kibaha mjini ambayo imendaliwa  mahususi kwa ajili ya kutekeleza ahadi yake ambayo aliitoa  ya kuwa na   darasa la kutoa  elimu ya ujasiriamali na jinsi ya kutengeneza bidha  bila malipo  ambapo ameanza mafunzo hayo katika kata mbili za Msangani pamoja  na Mkuza.

Post a Comment

0 Comments