Na Victor Masangu, Kibaha
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu ameamua kuja na mpango kabambe kwa kushirikiana na wazazi na walezi lengo ikiwa ni kuboresha miundombinu bora ya kuwajengea ofisi walimu katika shule zote ili waweze kufundisha katika mazingira mazuri na yaliyo salama.
Meya ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za mahafali ya tatu ya kuhitimu wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Kanesa iliyopo katika Kata ya Kongowe Halmashauri ya Manisspaa ya Kibaha Mkoani Pwani na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wazazi, walezi, pamoja na wadau wa sekta ya elimu.
Amesema kwamba katika kuunga mkoni juhuzu za serikali ya awamu ya sita ameona kua umuhimu mkubwa sana wa kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo wazazi na walezi katika mambno mbali mbali ikiwemo suala hilo la kufanya ujenzi wa ofisi za walimu katika kila shule ambapo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwaweka walimu kufundisha katika mazingira salama na yenye ubora.
Aidha mstahiki Meya ameongeza kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na wazazi katika kutatua changamoto za miundombinu ya elimu, pamoja na kutafuta fedha ambazo zitaweza kufanikisha ujenzi wa uzio katika shule hiyo,
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya msingi Kanesa amebaimnisha kwamba kwa sasa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo suala la ukosefu wa samani pamoja ana uzio hivyo ameiomba serikali kulitafutia ufumbuzi suala hilo kwa lengo la kuwawezea mazingira mazuri walimu pamoja na walimu.
Naye mmoja wa wadau wa maendeleo katika sekta ya elimu Hafidhi Amiri amesema kwamba aatakuwa bega kwa bega na serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha anashirikiana kikamilifu katika kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaikabili shule hiyo lengo ikiwa ni kuboresha sekta ya elimu.
Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi wapatao elfu 129 wameweza kuhitimu masomo yao ya darasa la saba katika shule hiyo ya msingi Kanesa iliyopo kata ya Kongowe Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.
.jpg)

0 Comments