MAKONDA AKAGUA MAENDELEO YA MABORESHO YA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA





Katika kuelekea mashindano ya AFCON 2027, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, Oktoba 18, 2026, amefanya ukaguzi wa maendeleo ya maboresho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, akiambatana na mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba.

Katika ukaguzi huo, Waziri Makonda alipokea taarifa kutoka kwa mkandarasi kuhusu hatua iliyofikiwa katika maboresho ya sehemu ya kuchezea ya uwanja huo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha miundombinu ya michezo inaboreshwa na kukidhi mahitaji ya mashindano makubwa ya kimataifa.

Maboresho hayo ni miongoni mwa hatua muhimu zinazochukuliwa kuelekea maandalizi ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), yatakayofanyika kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya na Uganda.

Post a Comment

0 Comments