NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amekagua maendeleo ya miradi ya utalii ikolojia katika Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia ya Pugu-Kazimzumbwi, inayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), iliyopo Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 20, 2026. Miradi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kwa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), inayowezeshwa kupitia Tozo ya Maendeleo ya Utalii (Tourism Development Levy – TDL).
Katika ziara hiyo, Waziri Kijaji amekagua ujenzi wa cottages na miundombinu saidizi, miundombinu ya burudani pamoja na mabanda ya kupumzikia watalii katika eneo la Bwawa la Minaki. Aidha, amezungumza na watumishi wa hifadhi hiyo kuhusu utekelezaji wa shughuli za utalii ikolojia na maendeleo ya miradi hiyo.
Uwekezaji huo unalenga kuboresha miundombinu na huduma za utalii, kuongeza mvuto wa Hifadhi ya Pugu-Kazimzumbwi na kuimarisha uwezo wa Tanzania kupokea wageni wakati wa AFCON, huku ukichangia kukuza utalii wa ndani na kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika uchumi wa Taifa.


0 Comments