WAZIRI ULEGA AWATAKA WATAALAMU KUSIMAMIA HAKI YA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI WANYONGE



Na Victor Masangu,Pwani
                              
Waziri wa katiba na sheria Mhe.Abdalah Ulega amewaagiza wataalamu wote  waliopangwa katika kampeni ya msaada wa kisheria  ya pili kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kutenda haki kwa wananchi bila ubaguzi wowote  hasa  kwa wale wenye uwezo mdogo pamoja na wale  ambao ni wanyonge waweze  kupatiwa haki zao zote kwa mujibu wa sheria na taratibu  za nchi

 Ulega ametoa kauli  hiyo wakati wa  ufunguzi  wa  kampeni  ya msaada wa kisheria ya Mama  Samia Legal Aid  awamu ya pili  katika Mkoa wa Pwani   ambao umefanyika katika viwanja vya stendi ya zamani maili moja Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa  serikali, viongozi wa chama, wabunge,taasisi wezeshi  pamoja wananchi.  

 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo  amesema kwamba kampeni hiyo itaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa maeneo ya pembezoni  ambao walikuwa wanakabiliwa  kwa kipindi kirefu na changamoto mbali mbali hususan migogoro ya ardhi kuweza kupata msaada wa kisheria bure hasa wanawake na watoto.


Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge  ya Utawala katiba  na sheria Mhe. Edwin Swale  amempongeza kwa dhati  Rais  wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hasssan  kwa  kuweza kuanzisha kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ambayo  kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa mbali mbali  kuweza kupata haki zao.


Kampeni  ya msaada wa kisheria ya Mama  Samia Legal Aid  awamu ya pili imezunduliwa rasmi   katika Mkoa wa Pwani  na Waziri wa katiba na sheria Abdalah Ulega na kwamba itakuwa ni mkombozi kwa mamilioni ya  wananchi  wa Tanzania katika masuala ya ardhi,miradhi, unyanyasaji wa kijinsia pamoja na utatuzi wa mambo mbali mbali.
                                                             

Post a Comment

0 Comments