TRA PWANI YATUA BAGAMOYO KUWEKA MIKAKATI NA WADAU WA FORODHA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO




Na Victor Masangu,Bagamoyo 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imekutana na wadau wa Forodha, hususan wafanyabiashara wanaojihusisha na uingizaji na usafirishaji wa mafuta ya kupikia kupitia Bandari ya Bagamoyo, kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kutafuta ufumbuzi wa pamoja utakaowezesha shughuli za biashara kufanyika kwa ufanisi.

Kikao hicho ambacho  kimefanyika   katika ofisi za TRA Wilaya ya Bagamoyo, kimekuwa sehemu ya jitihada za TRA kuimarisha mawasiliano na wadau wa Forodha, kutambua changamoto zinazowakabili na kujadili hatua za kuzitatua ili kuboresha mazingira ya biashara.

Akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani, Bw. Peter Jackson, amesisitiza kuwa TRA inaendelea kusimamia sheria na taratibu za Forodha huku ikiweka mazingira wezeshi kwa biashara halali. Ameeleza kuwa udhibiti wa bidhaa za magendo unafanyika kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali, na kusisitiza umuhimu wa kutoa elimu ya kodi na Forodha kwa wafanyabiashara.

Nao baadhi ya  wafanyabiashara wameishukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kuwapa nafasi ya kuwasilisha changamoto zao na kujadiliana namna ya kuzitatua. Wameeleza kuwa hatua hiyo imeimarisha mawasiliano na ushirikiano kati yao na TRA, huku wakitarajia mazungumzo ya aina hiyo kuendelea ili changamoto zinazojitokeza zipatiwe ufumbuzi kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments