Juma Duni Haji Mwenyekiti mpya Taifa wa Chama Cha ACT-Wazalendo
NA RASHID ABDALLAH, MCHAMBUZI,
TANZANIA
JUMA Duni Haji ama
'Babu Duni' anavyojulikana kwa wafuasi wake, ni mwanasiasa mtiifu wa upinzani.
Enzi za uhai wa Seif Sharif Hamad (almaarufu Maalim Seif) hadi anafariki,
hakukushuhudiwa mvutano wa hadharani kati ya Babu Duni na Maalim.
Yuko kwenye siasa za upinzani kwa takribani
miongo mitatu sasa. Ameshika nafasi mbalimbali za ndani ya Chama cha Wananchi
(CUF); Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha Taifa, Makamu
Mwenyekiti, na Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa.
Kuhama Vyama
Mwenyekiti huyo mpya wa ACT Wazalendo taifa,
alianza safari yake ya kisiasa muda mrefu. Tangu akiwa mwanafunzi katika skuli
ya sekondari ya Gamal Abdul Nasir, (sasa inaitwa Beit el Ras), alipokuwa
mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Afro-Shirazi Party (ASP).
Alifanya kazi kwa miaka mingi katika sekta ya
elimu Zanzibar akiwa Mwalimu na kushika nyadhifa mbalimbali katika taasisi
tofauti. Hizo zilikuwa ni nyakati akiwa ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ).
Baada ya kuunganishwa ASP na TANU Februari 5,
1977, na kupatikana Chama cha Mapinduzi (CCM), wanachama wa vyama hivyo viwili
wakawa wanachama wa chama kipya kilicholeta muungano wa kivyama kati ya
Tanganyika na Zanzibar.
Duni aliihama CCM baada ya mfumo wa vyama
vingi kurejeshwa kisheria Julai Mosi,1992. Kulikuwa na kundi la waasi wengine
walioikimbia CCM, ambao baadaye wakawa viongozi wa ngazi ya juu wa Civic United
Front (CUF), akiwemo Seif Sharif Hamad.
Amekuwa mgombea mwenza wa nafasi ya urais
mara nne upande wa Muungano wa Tanzania katika chaguzi za 1995, 2005 na 2010
akiwa na Profesa Ibrahim Lipumba. Mara zote CCM ikatangazwa mshindi.
Wakati wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Duni alihamia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa muda mfupi. Alikuwa mgombea
mwenza kwa mara ya nne katika uchaguzi wa 2015 WA Muungano, akiwa na Edward
Lowassa.
Ilipopatikana Serikali ya Umoja wa Kitaifa ,
Zanzibar baada ya uchaguzi wa 2010. Akiwa katika Baraza la Wawakilishi,
aliteuliwa kuwa Waziri wa Afya. Mbadiliko madogo ya baraza hilo 2014
yalimhamisha na kumpeleka Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.
Ulipovuma upepo wa kisiasa wa 'shusha tanga
pandisha tanga,' kufuatia mzozo mkali ndani ya CUF wanachama wa CUF walikihama
chama hicho wakiongozwa na Maalim Seif na kuhamia ACT Wazalendo, Machi 2019.
Juma Duni Haji alikuwa miongoni mwa waliohamia ACT.
Mfungwa wa Kisiasa
Novemba 1997, siku ya mwisho ya kampeni za
uchaguzi mdogo katika jimbo la Mkunazini, Unguja. Wafuasi kadhaa wa CUF
walikamatwa. Kamatakamata iliendelea hadi 1998, ambapo Duni naye alitiwa
mikononi mwezi Mei mwaka huo. Tuhuma zikawa ni kutaka kupindua serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Shirika la kutetea haki za binaadamu la
Amnesty International lilieleza wasiwasi wake katika ripoti kuwa wafungwa 18
wako ndani kutokana na maoni yao yasiyo ya vurugu na shughuli zao za kisiasa.
Ripoti hiyo ya Januari 2000 iliwaita wafungwa hao ni wa kisiasa.
Tuhuma zilizowakabili zilisababisha
kufunguliwa kesi ya uhaini. Duni alikaa gerezani kwa miaka miwili na nusu, na
baadhi ya wafuasi walikaa miaka mitatu huku kesi ikiendeshwa na Jaji Garba
Tumaka wa Nigeria.
Duni alishikiliwa tena baada ya maandamano ya
Januari 27, 2001, yaliyofanywa na wafuasi wa CUF, Unguja na Pemba, (chama kikuu
cha upinzani wakati huo). Msingi wa maandamano hayo ni kutoridhishwa na matokeo
ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000.
Mara hii kesi ya Duni ilikuwa ni tuhuma za
kuua Askari. Mwenyewe anaeleza ajabu ya kesi hiyo; ni kutuhumiwa kumuua Askari
aliyeko kisiwani Pemba wakati siku ya tukio Haji Duni alikuwa kisiwani Unguja.
Oktoba 15, 2001 Juma Duni Haji aliachiwa huru
baada ya mahakama kufuta kesi hiyo. Pia makumi ya wafuasi wengine waliokamatwa
katika maandamano walikuwa tayari wameachiwa huru miezi ya nyuma. Hatua hiyo
ilikuja kufuatia mazungumzo ya kisiasa kati ya CCM na CUF.
Historia ya siasa za Zanzibar ni za
panda-shuka, viatu mkononi. Duni amepita katika milima na mabonde ya siasa
hizo. Mwenyewe anaeleza hana tena cha kupoteza na kukaa kwake gerezani
kumemuongezea ujasiri.
Hatimaye Rais wa wanne wa visiwa hivyo aliyetawala kutoka 1990 - 2000,
Salmin Amour aliamuru waachiwe huru kabla ya uchaguzi mkuu 2000. Ifahamike pia
kuwa mwaka huo huo wa 2000 Mahakama ya Rufaa Tanzania ilitamka kupitia uamuzi
wake kuwa Zanzibar hakuwezi kutendeka kosa la uhaini kwani Zanzibar si Dola
(Sovereign State) bali ipo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Duni alishikiliwa tena baada ya maandamano ya
Januari 27, 2001, yaliyofanywa na wafuasi wa CUF, Unguja na Pemba, (chama kikuu
cha upinzani wakati huo). Msingi wa maandamano hayo ni kutoridhishwa na matokeo
ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000.
Mara hii kesi ya Duni ilikuwa ni tuhuma za
kuua Askari. Mwenyewe anaeleza ajabu ya kesi hiyo; ni kutuhumiwa kumuua Askari
aliyeko kisiwani Pemba wakati siku ya tukio Haji Duni alikuwa kisiwani Unguja.
Oktoba 15, 2001 Juma Duni Haji aliachiwa huru
baada ya mahakama kufuta kesi hiyo. Pia makumi ya wafuasi wengine waliokamatwa
katika maandamano walikuwa tayari wameachiwa huru miezi ya nyuma. Hatua hiyo
ilikuja kufuatia mazungumzo ya kisiasa kati ya CCM na CUF.
Historia ya siasa za Zanzibar ni za
panda-shuka, viatu mkononi. Duni amepita katika milima na mabonde ya siasa
hizo. Mwenyewe anaeleza hana tena cha kupoteza na kukaa kwake gerezani
kumemuongezea ujasiri.
@@@
0 Comments