RAIS SAMIA AZIDI KUKIPAISHA KISWAHILI DUNIANI

NA JOHN MAPEPELE

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan amesema Sera mpya ya mambo ya nje itaendelea kuzingatia pamoja na mambo mengine kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kidiplomasia.

Rais Samia alisema hayo wakati akizungumza na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao Januari 24, 2022 hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika  sherehe za mwaka mpya 2022 ( Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika   Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Samia aliwashukuru wote waliopitisha maazimio ya kuifanya tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya lugha ya Kiswahili duniani.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mohamed Mchengerwa alisema Wizara yake kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itahakikisha inasimamia maendeleo ya Lugha ya Kiswahili kwa faida ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu alifafanua kuwa Kiswahili ni miongoni mwa lugha kubwa duniani ambayo vyuo vikuu, vyombo vya habari na wananchi wa nchi mbalimbali duniani wamekuwa wakitumia katika mawasiliano.

"Lugha ya Kiswahili ni kitu ambacho kitaliletea uchumi mkubwa taifa letu, tumejipanga kuliletea  mapato makubwa taifa letu kupitia lugha hii” alisisitiza  Yakubu

Aliongeza kuwa kupitia BAKITA  mapinduzi makubwa yanakwenda kufanyika  ikiwa ni pamoja na kubidhaisha  lugha hiyo  duniani.“. 

Post a Comment

0 Comments