Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco
NA MWANDISHI WETU
KOCHA Mkuu wa Simba Pablo Franco, amesema ana imani kuanzia sasa timu itaanza kufunga mabao mengi wakianza na mchezo wa kesho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.
Pablo amesema kumekuwa na changamoto ya kupata mabao licha ya kutengeneza nafasi nyingi lakini tayari suala hilo limefanyiwa kazi mazoezini na kila kitu kiko sawa.
Akizungumzia mchezo wenyewe Pablo amesema utakuwa mgumu kutokana na ubora wa ASEC pamoja uzoefu wao lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda katika uwanja wa nyumbani wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
“Ninaamini tutaanza kupata mabao mengi, tumekuwa tukifanya mazoezi sana kuhusu ufungaji na kila kitu kitakaa sawa kuanzia kesho,” amesema Pablo.
0 Comments