ACT-WAZALENDO YAITAKA SERIKALI KUFUTA TOZO ZA MIAMALA YA SIMU

Msemaji wa Sekta ya Fedha na Uchumi wa ACT-Wazalendo Emmanuel Mvula akiwasilisha uchambuzi kuhusu hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/2023 jijini Dar es Salaam.


Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zito Kabwe akizungumza wakati wa uwasilishaji wa uchambuzi kuhusu hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

NA ABRAHAM NTAMBARA

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka Serikali kufuta tozo za miamala ya simu ili kuwapunguzia mzigo wananchi.

Hayo yamebainishwa leo Juni 16, 2022 jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Sekta ya Fedha na uchumi wa ACT-Wazalendo Emmanuel Mvula wakati akiwasilisha uchambuzi kuhusu hotuba ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 iliyosomwa bungeni juzi na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchema juzi.

Mvula amesema lengo la kuondoa tozo hizo ni kurudisha ili irudi kama ilivyokuwa kabla ya mwezi Julai mwaka 2022 ili kuwapunguzia mzigo.

“Tulionya kuwa tozo za miamala ya simu zitaongeza maumivu maumivu makubwa kwa wananchi. Makusanyo yake kuwa chini ya malengo, inadhihiri, tozo ni mzigo usiobebeka kwa walipa kodi. Hivyo kupelekea kushuka kwa kwa huduma za miamala ya simu,” amesema Mbvuula na kueleza kwamba,

“Katibu Hotuba ya Bajeti ya Serikali 2022/2013. Serikali imesema itapunguza, kakato/ada za miamala ua ya simu kwa asilimia 48. Punguzo hili haliwezi kuleta manugaa kwa wananchi,”.

Aidha amesema mwaka 2018 Serikali ilipora mapato yatokanayo na   ushuru wa wa mauzo ya nje ya Korosho ghafi yaani Export Levy.

Kwamba Serikali ilibadili sheria ya na kuchukua asilimia 100 ya mapato ya ushuru huu kwa ahadi kuwa Serikali ndiyo itakayo hudumia gharama zote na haikufanya hivyo.

“Kabla ya Serikali kuanza kupora ushuru wa mauzo ya nje kwa korosho, asilimia 65 ya mapato yatokanayo na ushuru huo yalikuwa yanarudi kwa wakulima kupitia mfuko wa kuendeleza zao la korosho.

Mvula akichanganua bajeti hiyo ya zaidi ya shilingi trioni 41, amesema bajieti ya mwaka 2022/2023 sehemu kubwa itatumiwa kulipa mashahara, kugharamia deni la Serikali, pamoja na matumizi mengine, huku asilimia 49 tu ya bejeti ya fedha zote za bajeti ndiyo inakwenda kwenye kuhudumia za wananchi.

@@@@

Post a Comment

0 Comments