NA MWANDISHI WETU
JAMII imetakiwa kutoa taarifa mapema za watoto wanapozaliwa na tatizo la Mguu Kifundo.
Kauli hiyo imetole leo Juni 3, 2022 jijini Dar es Salaam na Dkt. Frank Erabi wa kitengo cha mifupa katika Taasisi ya CCBRT Tanzania, ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya Mguu Kifundo yaliyofanyika katika Taasisi hiyo.
“Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni "Mguu Kifundo unatibika muwahishe mtoto hospitalini", ni ukweli usiopingika kuwa tatizo la mguu pinde au Mguu Kifindo unatibika kitu muhimu zaidi baada ya mazazi kugundua kuwa mtoto ana tatitizo hilo inashauriwa kurudishwa hospitalini ndani ya wiki mbili na kabla ya miezi mine,” amesema Dkt. Erabi.
Dkt. Erabi ameongza kwamba tatizo la Mguu Kifundo linatibika na mtoto kuwa katika hali nzuri kama watoto wengine kwamba kitu cha kuzingatia ni mzazi kuwahi hospitalini ambapo atapatiwa matibabu ikiwemo upasuaji mdogo na kupatiwa viatu maalum na ndani ya muda mfupi atakuwa amerejea katika hali ya kawaida kama binadamu wengine.
Kwa upande wake
Mfiziotherapia wa CCBRT Dkt. Cosmas Daud amesema kuwa maadhimisho hayo
hufanyika kila mwaka Juni 3 kama sehemu za kuenzi jitihada za mfadhili na
mgunduzi wa tiba za Mguu Kifundo anayefahamika kwa jina la Moralfeet kutoka
Amenia.
“Tanzania ilianza kutoa matibabu hayo 2008 bila malipo kwakuwa mgunduzi wa tiba hiyo ya Mguu kafindo ndiye mfadhili hivyo tunasisitiza kuwa huduma hii tunaitoa bure na Watoto wanapazaliwa na tatizo hili waletwe CCBRT tumedhamiria kuwatibu na kuwapa furaha ya maisha,” amesema Dkt. Daudi wa Kitengo cha Fiziotherapia.
Kwa mujibu wa Dkt. Daudi hadi sasa hakuna sababu za Moja kwa Moja zilizogundulika kuwa ndiyo chanzo cha tatizo hilo ispokuwa zile ndogondogo na za kukisiwa kuwa huenda mtoto alikaa vibaya, Mila desturi, kichwa kikubwa, mgongo wazi na mengineyo.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani kila mwaka watoto 750,000 hadi 800,000 huzaliwa na tatizo la Mguu kifundo.Kwa Tanzania watoto 2500 hadi 3000 huzaliwa na tatizo hilo na CCBT hutibu watoto wasiopungua 350 hadi 400 kwa mwezi.
Zaina Othman mkazi wa Pugu ambaye mwanaye wa miezi miwili aliyekuwa akihudhuria kliniki yake katika hospitali hiyo aliishukuru CCBRT kwakurekebisha miguu yake miwili kuwa katika hali ya kawaida.
“Kwanza ni
mshukuru Mung una uongozi wa CCBRT ambao hutoa huduma hii bure bila ubaguzi
mwanangu niligundua kuwa ana tatizo hilo baada ya wiki mbili na wiki ya tatu
nimemleta hospitalini leo ana miezi miwili tunahudhuria Kliniki ya kawaida
“alisema Zaina mama Sahili Omary.
Naye Hadija Said Mkazi wa Kimara mwenye mtoto Jumanne Omary (4 na miezi 10) ambaye mwanaye alirekebishwa miguu yake CCBRT aliliambia CCBRT kuwa ipo haja taarifa za huduma hizo kwenda mbali zaidi kwakuwa kuna Watoto wengi wanazaliwa hususani vijijini na tatizo hilo lakini hawajui pakuanzia”alisema Hadija
“Wengi hawana taarifa ya matibabu haya kuwa hutolewa bure lakini pia mara mzazi anapogundua tatizo hilo aende kwa wataalamu wa afya badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji wakidhani wamerogwa”alisema mzazi wa Jumanne Omary.
Hospitali hiyo tokea kuanzishwa kwake imetimiza miaka 28 ya utoaji huduma za tiba kwa watoto wenye matatizo ya macho, miguu pinde, mgongo wazi na afya ya uzazi ikiwemo fistula.
0 Comments