Masanii wa Musiki wa Singeli ambaye awali alikuwa akiimba musiki wa Taarab Mwajuma Cheupe akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam baada ya kutambulishwa kama msanii wa kwanza wa Peaktime Music Label.
NA ABRAHAM NTAMBARA
PEAKTIME Music Label imemtambulisha msanii wake wa kwanza Mwajuma Kingongo maarufu kama Mwajuma Chaupepo ambaye amekuja na ujio mpya wa kuimba musiki wa Singeli.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati wa kutambulisha msanii huyo Mratibu wa Matukio wa Peaktime Music Label Bakari Khatibu amesema Label hiyo imeamua kusapoti vijana wenye vipaji kwani music ni ajira.
Amesema Label hiyo itakuwa ikisimamia na kuratibu shughuli mbalimbali za music kwani kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiratibu tu mapambano ya ngumi.
“Hivyo tumeona ni vizuri kuanza kusapoti pia kwenye muziki wa Singeli na hapa tunamtambulisha msanii Wetu wa kwanza kwenye Label yetu Mwajuma Chaupepo,” amesema Khatibu.
Kwa upande wake msanii huyo Mwajuma Chaupepo ambaye awali alikuwa akiimba musiki wataarab ameishukuru Peaktime Music Label kwa kutambua kipaji chake na hatimaye kumuweka chini ya Label hiyo akiwa ni msanii wa kwanza.
“Awali nilikuwa nikiimba musiki wa taarab na sasa nimevamia kwenye kuimba Singeli na nipo hapa kama msanii wa kwanza kwenye Label hii. Hivyo nishukuru kwa kutambuliwa na kujiunga na Label hii,” amesema Mwajuma.
Ameahidi kwamba atafanya kazi kubwa kwa moyo na nguvu ili kuhakikisha haiangushi Label hiyo na kuwataka wasanii wengine kuhakikisha wanajiunga na Label ya Peaktime Music.
Katika hatua nyingine Mwajuma Chaupepo ametangaza ujio wa EP yake inayojulikana kama “Kula Ushibe” yenye nyimbo saba (7) ambayo ataizindua Juni 17 mwaka huu.
Kwamba katika uzinduzi huo atakuwa na wasanii wengine ambao amewashirikisha kwenye EP yake.
0 Comments