JMAT YAANDAA MATEMBEZI YA AMANI, WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWA MGENI RASMI


Mwenyekiti wa Machifu Tanzania Antonia Sangalali akizungimza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

NA ABRAHAM NTAMBARA

JUMUIYA ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imeandaa matembezi ya Amani yatakayofanyika Desemba 2 Mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa Novemba 21, 2023 na Mwenyekiti wa Machifu Tanzania Antonia Sangalali akizungimza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Chifu Sangalali amebainisha kuwa matembezi hayo yatahudhuriwa na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Amesema lengo la matembezi hayo ni kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuongoza kwa Amani na utulivu.

Amesema Nchi bila Amani hakuna chochote kinachoweza kufanyika Kwamba Amani ni kitu muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote lile.

Ametumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyeki wa JMAT Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salam kwa ubunifu wake huo wa kuandaa matembezi hayo.

Post a Comment

0 Comments