MWINJILISTI TEMBA ALIA NA AJALI MOROGORO ROAD, AMWELEZA UKWELI RAIS DKT. SAMIA



NA ABRAHAM NTANBARA

MWINJILISTI Alphonce Temba amesema sababu ya ajali zinazotokea katika barabara ya Morogoro (Morogoro Road) kuanzia Mlandizi hadi chalinze ni kutokana na kuzidiwa kwa barabara hiyo.

Amebainisha hayo leo Novemba 22, 2023 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya kadhia hiyo ya ajali ambayo imekuwa ikichukua uhai wa watu wengi.

“Nataka nimwambie Rais, watu wanakufa kwa sababu barabara ya Morogoro Road kuanzia Mlandizi hadi Chalinze barabara ni finyu imezidiwa, kwahiyo madereva wanapo overtake kidogo lazima kuwe na ajali,” amesema Mwinjilisti Temba.

Ameeleza kuwa katika barabara hiyo Trafiki wamekuwa hawashughiliki na speed mita za mabasi, hivyo amewaomba Mawaziri wa Uchukuzi na Waziri wa Ujenzi kufahamu hilo ili kufanyike upanuzi wa barabara hiyo.

Amesisitiza kuwa kutokana na ufinyu wa barabara hiyo vifo vingi vimekuwa vikitokea.

“Ajali zinazotokea kuanzia Mlandizi mpaka Chalinze inatokana na ufinyu wa barabara na sio mwendokasi, naomba mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia, ajue hilo,” amesisitiza Mwinjilisti Temba.

Hivyo amesema ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo Mwinjilisti Temba ameshauri Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) ili barabara ipanuliwe.

Vile vile ameshauri kwa barabara ya Morogoro Road kuanzia Mlandizi hadi Chalinze Serikali ifanya upanuzi wa barabara hiyo hivi sasa.

 

Post a Comment

0 Comments