TAMTILIA MPYA YA “SIRI” KUONYESHWA KWA MARA YA KWANZA DESEMA MOJA MWAKA HUU KWENYE CHANELI YA SINEMA ZETU



NA ABRAHAM NTAMBARA

MSANII nguli wa Filamu nchini Irene Paul kwa kushirikiana na Wasanii wengine mahiri wanaotamba na katika tasnia hiyo kama Prince Jimmy, Habib Mtambo, Neema Wale, Zai Kijiwenongwa na wengine wengi watafungua pazia la burudani za msimu huu wa sikukuu kwa tamthilia kali inayojulikana kama SIRI.

Hayo yamebainishwa na Masimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu Sophia Mgaza akizungumza katika hafla ya kutambulishwa kwa tamthilia hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“SIRI itaonyeshwa kwa mara ya kwanza tarehe 1/12/2023 katika Chaneli ya Sinema Zetu (Chaneli 103) kwenye kisimbuzi cha Azam TV kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili Saa moja na Nusu usiku, yaani siku tatu mfululizo kila wiki, pia unaweza kuendelea kufuatilia Tamthilia hii kiganjani kwako kupitia AzamTV Max App,” amesema Mgaza.

Amebainisha kuwa Tamthilia hii umeandaliwa na Godly Production chini ya muandaaji mpya katika ulimwengu wa Tamthilia Irene Paul.

Kwamba miongozi mwa waigizaji mashuhuri katika Tamthilia hiyo ni pamoja na Irene Paul mwenyewe, Neema Walele, Habibu Mtambo, Prince Jimmy, Salha Abdallah, Salim Yakuti, Mayasa Mrisho, na Zainab Ally maarufu kama Zai Kijiwenongwa.

Wengine ni Shafii Bashiri, Christina Rogat na Wasanii wengine wengi wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Tanzania.

Mgaza ameeleza kuwa Tamthilia hiyo inachukua nafasi ya Tamthilia ya Mchongo inayofikia tamati Novemba 25, 2023.

 

Post a Comment

0 Comments