MKURUGENZI WA TCAA ATOBOA SIRI YA KUBEBA TUZO ZA ATE.



Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari amesema usimamizi mzuri wa Rasilimali watu, kuwawekea maslahi mazuri wafanyakazi pamoja na kuimarisha mifumo ndio sababu iliyoifanya mamlaka hiyo kutwaa tuzo ya pili ya Taasisi za Umma, zinazotolewa na Chama cha waajiri nchini(ATE).

Johari ametoboa siri hiyo leo jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mlimani city jijini hapa wakati wa utoaji wa tuzo kwa waajiri bora mwaka 2023.

Aidha,Johari amesema tuzo hiyo itakuwa chachu kwao TCAA kuzidi kwao kuboresha huduma.

"Nafurahi kwa ushindi huu wa pili kwa taasisi za umma yote inatokana na kuimarisha mifumo,kusimamia Rasilimali watu pamoja kuwawekea maslahi mazuri wafanyakazi wetu"Amesema Johari.

Hata hivyo,Johari amesema katika tuzo taasisi zaidi elfu moja zilijitosa huku 94 ndio zilikizi vigezo na taasisi 14 ndio ziliibuka ushindi.

Kadhalika,Johari,amehaidi mwakani wanatarajia kushika nafazi kwanza kwenye tuzo hizo kutokana na TCAA kutoa huduma bora.

Post a Comment

0 Comments