MBUNGE MSHASHU AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UTENDAJI ULIOTUKUKA.


Na Lydia Lugakila, Bukoba

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Bernadeta Kasabago Mshashu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu hassan kwa jinsi alivyoupenda Mkoa wa Kagera na kuupatia mabilioni ya pesa ambayo yameuwezesha Mkoa huo kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi.

Mshashu ametoa kauli hiyo katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa -RCC kilichofanyika Februari 19,2025 katika ukumbi wa Mkoa huo.

"Tumeona kazi kubwa aliyoifanya Rais wetu tumeona miradi mingi ya kimkakati   tunampongeza Rais Samia hakika ametuheshimisha Kagera"alisema mbunge huyo.

Mshashu Amempongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajat Fatma Mwassa kwa kazi anazozifanya wakiwemo wakuu wa Wilaya pamoja na watendaji mbali ambao wemeweka juhudi zao katika kuuinua Mkoa huo ki uchumi.

Hata hivyo aliwaomba Wana Kagera kuendelea kushirikiana vyema katika mambo mbali mbali ya kuuinua Mkoa huo kiuchumi

Hata hivyo Ameongeza kuwa Wanakagera na Watanzania kwa ujumla tuzidi kumuombea Rais Samia ili apate kuiongoza Nchi kwa kipindi kingine.

Post a Comment

0 Comments