MSIGWA: MAUZO YA KAHAWA KUFIKIA BILIONI 1 IFIKAPO 2030, uzalishaji kuongezeka hadi Tani laki tatu


Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa 

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imesema kuwa inatarajia ifikapo 2030 mazuzo ya zao la Kahawa yatafikia Dola bilioni Moja (1) na uzalishai ifike Tani laki tatu.

Hayo yamebainishwa leo Februari 19, 2024 na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa akizungumza kwenye Cafe Talk na vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia mkutano wa 3rd G25 African Coffee Summit unaotarajiwa kufanyika Februari 21 na 22 Mwaka huu.

"Tunatarajia tufike mauzo ya Dola Bilioni 1 itakapofika 2030. Na tunataka uzalishaji wa kahawa ufike tani laki tatu na hii ni kahawa tu na zipo kazi kubwa za kimkakati zinafanyika kwa ajili ya Kahawa," amesema Msigwa na kuongeza,

“Nchi yetu ni ya nne (4) kwa uzalishaji wa Kahawa Afrika na mauzo yetu sisi kwa sasa ni Dola milioni 240 na ni kazi ambayo imefanyika kwa miaka mitatu (3) ya Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani na kuongeza uwekezaji kwenye kilimo,".

Kwamba zao la Kahawa kwa Afrika ni za la kimkakati hivyo Serikali imeweka mikakati bora zaidi kuhakikisha kuwa changamoto za wakulima zinatatuliwa na wanazalisha Kwa wingi na ubora unaotakiwa Kimataifa.

Kuhusu kumbi za mikutano amesema kuwa Serikali inataka kufungua mikoa mingine kiuchumi na sehemu mbalimbali lakini haiwezi kujenga kituo cha mikutano sehemu ambazo hakuna viwanja vya ndege, wala  hoteli za kulala wageni.

Hata hivyo amesema uwepo wa kumbi za mikutano katika mikoa mingine ni la muhimu  hivyo katika mikoa mingine yote wataendelea kupeleka huduma taratibu ili kupanua wigo wa huduma mbalimbali kuwafikia wananchi wote na kuitangaza Tanzania.

“Mikutano hii tunayoiona ni namna Rais alivyoamua kutekeleza Diplomasia na Rais alisema anataka kuifungua nchi na moja ya namna ya kuifungua nchi ni pamoja na mikutano hii. Na mikutano mikubwa ndio inayotangazwa zaidi lakini niseme mikutano midogo ya Kimataifa ambayo inafanyika Tanzania ni mingi sana," ameeleza Msigwa.

Msigwa amesema kwa sasa Serikali inataka kujenga ukumbi mwingine mkubwa sana ambao utaitwa Kilimanjaro International Convention Center na ukumbi huu utaweza kuingiza watu 3000 au 5000.

"Kwa sasa kuhakikisha watu 5000 wanakaa pamoja ni changamoto na tutajenga kituo hiki pale Arusha. Utalii wa mikutano ni mkubwa," ameeleza Msigwa.

Post a Comment

0 Comments