SAMIA CUP 2025 YAZINDULIWA RASMI VIWANJA VYA MJI MWEMA KIGAMBONI, timu 32 kutifuana kukisaka kikombe cha ubingwa.



NA MWANDISHI WETU

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ACP John Malulu amezindua mashindano ya Samia Cup 2025 katika viwanja vya Mji Mwema Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza Wakati wa Uzinduzi wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Twende Pamoja na Mama Sports Promotion uliofanyika jana katika viwanja hivyo ACP Malulu alisema lengo la Samia Cup 2025 ni kuibua vipaji na kufurahia burudani.

"Jeshi la Polisi Temeke, tunasema michezo ni Afya, upendo na matokeo ya Amani, bila amani hakuwezi kuwa na kusanyika kama hili. Hivyo kama Jeshi tunatumia michezo kuwafikia vijana na jamii kupenyeza na kueneza maneno ya uzalendo na upendo kuhakikisha Nchi inakuwa na Amani," alisema ACP Malulu na kuongeza,

"Hivyo tutumie mashindano haya kumuunga kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda na kutunza Amani ya Nchi,".

ACP Malulu aliwahakikishia uwepo wa Amani washiriki wa mashindano hayo hadi yatakapotamatika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Twende Pamoja na Mama Sports Promotion na Mkurugenzi wa Makunduchi Villa Motel Mohammed Haji alisema mashindano hayo yanashirikisha timu 32 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema mashindano hayo yanafanyika ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia katika kukuza na kuendeleza Sekta ya michezo nchini kwani michezo ni ajira.

Kwamba ligi hiyo iliyoanza Februari 7, Mwaka huu itadumu Kwa kipindi cha miezi miwili.

Naye Mratibu wa Mashindano hayo Omary Kombo alisema mashindano hayo yatasaidia katika kukuza na kuendeleza michezo.

Post a Comment

0 Comments