NA MWANDISHI WETU
WASANII wa Filamu na Muziki ambao ni Mabalozi wa Mama, wamesema watazunguka Nchi mzima kutangaza mazuri yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kampeni yao ya "ASANTE MAMA".
Hayo yamebainishwa na Msanii wa Filamu nchini Jimmy Mafufu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alitumia fursa hiyo kueleza kuwa yeye pamoja na Msanii mwenzake Shamsa Ford wameamua kujiunga na Chama cha Mapinduzi wakiachana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Nyota huyo wa filamu nchini wameamua kujiunga CCM wakitokea Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) wanakiri sababu kubwa ya kuchukua uamuzi huo ni kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na Dkt Samia ambayo inafanya taifa kukua kiuchumi.
Mafufu amesema wameamua kuijunga na CCM baada ya kubaini kupitia Serikali ya Awamu ya Sita imefanya makubwa kwa Watanzania wakiwemo wasanii ambao wamepewa mikopo ya kuinua kazi zao.
“Licha ya kwamba mimi na Shamsha tulikuwa upinzani, mikopo hiyo inayotolewa na Rais wetu kwa wasanii haikutubagua, pia Serikali yetu imefanya mambo makubwa ikiwemo utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo kama Barabara, Bwawa la Mwalimu Nyerere, Reli ya SGR, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato, hayo ni sehemu yaliyotukusukuma kujiunga CCM,” amesema.
Amesisitiza kwamba tangu Rais Dkt Samia, aingie madarakani hajashindwa, ametekeleza miradi yote iliyoachwa na marehemu Rais Dkt John Magufuli, hali ambayo imefanya kutoona umuhimu wa kuwa wapinzani.
Wasanii hao wameungana na wasanii wengine akiwemo Salum Mchoma (Chiki), Single Mtambalike ‘Richt Ritch’, Rashidi Mwishehe ‘Kingwendu’ Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’ na wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Boniventure Kabongo ‘Stamina, Juma Kassim ‘Nature ‘Sir Nature’, Amani Temba ‘Capt Temba, Richard Shauri ‘Ritch One’ na wengine na lengo lao ni kutangaza miradi yote ambayo imetekelezwa chini ya Rais Samia.
Shamsa naye amesema kwamba anajivunia kujiunga na CCM na kutoa wito kwa wasanii wengine ambao wako katika vyama vya upinzani kujiunga na ccm ili kuunganisha nguvu ya pamoja kutangaza miradi ya maendeleo ambayo imefanikisha kustawisha uchumi wa Tanzania.
Pia Ritch Ritch ambaye ni diwani wa CCM katika Kanda ya … amesema kuwa yeye ndiye kiongozi wa madaiwani wote hivyo anaamini watatangaza, miradi yote ambayo imefanya vizuri kwa maslahi ya watanzania ili kila mmoja ajue namna Serikali ambayo imefanikio ikiwemo miradi ya Elimu, Usafiri wa Anga na mingineyo inayofanya Tanzania kuwa mfamo wa kuigwa katika mataifa mengine.

0 Comments