Mbeto: OMO hajawahi kuwa mpiga kura Zbar


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Idara ya Itikadi, Uenezi na Mfunzo ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, imemtaja  Mwenyekiti  wa ACT ,Othman Masoud Othman , hakuwahi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga kura na wala kuwa mpiga kura mwaka wowote . 

Mara kadhaa,  CCM kimemtaja  Othman  si kwamba hajawahi kujiandikisha tu ,lakini pia hakuna rekodi inayoonyesha kama amewahi kupiga kura  katika jimbo lolote.

Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar ,Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, alisema jina la Othman  ,halionekani katika orodha ya wapiga kura walioandikishwa  kuanzia mwaka 1995 hadi 2025 .

Mbeto  alisema kilichofanyika huko Mpendae , amekwenda   kujiandikisha  na kama mpiga  kura mpya , wakati  zoezi  la wapiga kura kuhakiki na  kurekebisha taarifa zao  limeshafanywa  na Tume ya Uchaguzi Zanzibar  (ZEC) Julai Mwaka 2020.

Alisema kutoonekana  jina la Othman katika  orodha ya wapiga kura  wa zamani, kunaweza kuthibitisha  kuwa kiongozi  huyo hajawahi kumpigia kura mgombea  urais kwa tiketi  ya ACT  Hayati Maalim  Seif  

"Si jambo la kupepesa maneno ila ni  rahisi   kusema Othman ni aina ya kiongozi asiye na msimamo. Si kosa kisiasa  akitwa mwemye rangi za mwanasiasa kinyonga au  mchumia tumbo "Alisema Mbeto 

Katibu  huyo Mwenezi  alisema madai yaliotolewa na Jussa na kudai  Hayati Maalim  Seif Sharif Hamad  , ndiye aliyempendekeza Othman kurithi  uongozi  wa ACT , ni mbinu batili na  uongo mtupu . 

"Hawezi kupemdekezwa mtu ambaye hakushiriki harakati  zozote  za kuijenga CUF au ACT. Othman amidandia siasa za ACT kwa mbinu  na mizengwe ilizosukwa na Jussa akiwa na wenzake  wake saba "Alieleza 


Aidha Mbeto  aliongeza kusema hata katika jimbo la Mpendae, Othman amenunua nyumba tu lakini kwa miaka yote hakuwahi  kuwa  Mkaazi wa kuduumu wa eneo hilo kama sheria  ya Ukaazi Namba 4 ya mwaka 2018 inavyoelekeza .

"OMO amekosa  hata  sifa ya  kuwa mpiga kura mpya .Huu si wakati wa kurekebisha  tarifa walioandikishwa  kupiga  kura .Kwa muktadha huo hakuwahi kumchagua hata aliyekuwa  bosi wake Rais Mstaafu Dk Ali Mohamed Shein wala  Maalim  Seif  "Alieleza  .

Akizungumzia madai  yaliowahi kutolewa na Jussa huku  akisaidiwa na mjane wa Maalim Seif,  Bi Awena Sinani, ikidaiwa kuna  usia ulioachwa na Hayati  Maalim  Seif  , unaomdekeza Othman awe kiongozi ACT jambo hilo ni uzushi  mtupu  

"Ni lazima vyama vyetu viwe makini kudhibiti   viongozi matapeli  wa kisiasa.Huenda ameihukumu sana  SMZ na sasa  anakitafuna "Alisiaitiza Mbeto  

Hata hivyo hata Hati ya kusafiria ya OMO haionyeshi kama mwaka 2020 aliwahi kusafiri na kukaa nje ya Zanzibar  zaidi ya miaka mitatu hivyo  bado anaonekana kutothibitika kuwa mpiga kura halali.

Post a Comment

0 Comments