OMO AWASILI NCHINI AKITOKEA AFRIKA KUSINI.....


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Machi 15, 2025, amewasili nchini Tanzania akitokea jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, alikopitia akitokea Angola.

Akiwa kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa O. R. Tambo jijini Johannesburg, Mheshimiwa Othman alisindikizwa na kuagwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Balozi James G. Bwana. 

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Mhe. Othman amepokelewa na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ndugu Ado Shaib Ado.


Kitengo cha Habari 
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Machi 15, 2025.

Post a Comment

0 Comments