SERIKALI YAZIDI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI YA UWEKEZAJI


*#KAZIINAONGEA*

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amefanya ziara katika kongani ya viwanda Kwala (Sino Tan)  pamoja na bandari kavu iliyopo Kwala Mkoa wa Pwani. 

Ziara hiyo iliyohusisha waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, imelenga kuonesha juhudi za Serikali katika kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji sambamba na uboreshwaji wa miundombinu na Bandari zilizopo nchini.

Mradi wa Hifadhi ya Viwanda ya Sino-Tan, ni moja ya mradi wa kimkakati katika Wilaya ya Kwala, Mkoa wa Pwani, unaolenga kubadilisha taswira ya viwanda nchini kupitia viwanda vikubwa na vya kati 200 na vidogo 300. Miongoni mwa viwanda hivyo ni pamoja na usindikaji wa vyakula, utengenezaji wa vifaa, viwanda vya dawa, vifaa vya ujenzi, usindikaji wa viatu na nguo, na viwanda vya kemikali.

Mradi huo umefanikiwa kwa Awamu ya kwanza ya  imekamilika kwa 80%. Miundombinu muhimu kama barabara, mtandao wa umeme, na maji tayari viko imara ndani ya eneo la mradi.

Sambamba na suala la Ajira na Uchumi, Hifadhi hii inatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 500,000, na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa hadi dola bilioni 6 za Kimarekani na kuongeza mapato ya kodi ya TZS Trilioni 1.2 kila mwaka.

Vilevile katika suala la Uwekezaji wa Serikali, Serikali inaendelea kuwekeza katika miundombinu kama barabara za zege, mtandao wa fiber optic, na usambazaji wa umeme na maji kutoa msingi thabiti kwa uzalishaji wa viwanda.

"Tunajivunia maendeleo haya na tunaamini kuwa mradi huu utakuwa kitovu cha viwanda kinachovutia uwekezaji zaidi na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania". Msigwa amesisitiza

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments