TANZANIA KUIUZIA UMEME ZAMBIA



#KAZIINAONGEA 

Tanzania imefanya mazungumzo ya makubaliano makubwa ya kuiuzia nchi ya Zambia umeme wa hadi megawati 1000 kwa mwaka, kupitia mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kanona Power (T) Limited, kampuni tanzu ya Kanona Power Company Limited kutoka Zambia. 

Imebainishwa kuwa ikiwa mazungumzo hayo yatafanikiwa, basi mkataba utakaosainiwa unatarajiwa kuingizia TANESCO mapato ya takriban Dola bilioni 1 (TZS trilioni 2.5) na kuongeza mchango wa sekta ya nishati kwenye uchumi wa Tanzania.

Aidha, ikiwa mazungumzo hayo yatafikia makubaliano, Kanona Power itajenga njia ya kusafirisha umeme ya kV 220 kutoka Mwakibete, Mbeya hadi Nakonde, mpakani mwa Tanzania na Zambia. 

Hatua hii inalenga kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa wakati huku ikisaidia mahitaji makubwa ya nishati kwa nchi jirani.

Halikadhalika Kanona Power, ambayo kwa sasa inasambaza umeme kwa kampuni kubwa ya madini nchini Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), inatarajia kuanza kununua umeme kutoka TANESCO kwa awamu.

*#Kazi na Utu,Tunasonga Mbele*

Post a Comment

0 Comments