NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Jumuiya ya Wanakwe wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Tawi la Boko Clara Bundu amechukua fomu ya kutia nia kuwania udiwani wa Viti Maalum Kata ya Bunju, Tegeta Halmashauri ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 29, baada ya kukabidhiwa fomu hiyo ameomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kumpatia na fasi ili kuwatumikia wananchi.
Amesema hadi leo yeye ni mwanamke pekee kwa Kata ya Bunju aliyejitokeza kuchukua fumo kumba ridhaa hiyo.
Mgombea huyo amechukua fomu katika ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, ambapo amekabidhiwa na Katibu wa UWT wa Wilaya hiyo, Haziati Juma.
0 Comments