NA MWANDISHI WETU
Mweneyekiti wa Jumuiya ya Wanakwe wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Shina namba 13 Bunju B Mkoa wa Dar es Salaam Grace Mushi amechukua fomu ya kutia nia kuwania udiwani wa Viti Maalum Kata ya Mabwepande Halamshauri ya Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 29, 2025 baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Mushi amesema lengo ni kutaka kupambania maendeleo ya wananake.
Hivyo ameomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kumpatia na fasi ili kuwatumikia.
Mgombea huyo amechukua fomu katika ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, ambapo amekabidhiwa na Katibu wa UWT wa Wilaya hiyo, Haziati Juma.
0 Comments