DKT. NCHEMBA AITAKA BODI YA BoT KUENDELEA KUSIMIA MISINGI YA KUANZISHWA KWAKE


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuendelea kusimamia misingi ya kuanzishwa kwa Bodi hiyo wakati wa mkutano na ujumbe wa Bodi hiyo ukiongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba (Kulia), ambapo umeeleza mafanikio ya Benki likiwemo suala la kuendelea kuimarisha uchumi, jijini Dodoma.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Emmanuel Tutuba akieleza mafanikio ya Benki hiyo katika kuimarisha uchumi wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambapo aliongoza ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo ambao umeeleza mafanikio yaliyopatikana likiwemo suala la kuendelea kuimarisha uchumi, jijini Dodoma.

Na. Peter Haule, WF, Dodoma

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ukiongozwa na Gavana wa Benki hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba, ambapo umeangazia mafanikio ya Benki hiyo katika kuendelea kuimarisha uchumi.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, Dkt. Nchemba aliitaka Bodi hiyo ya Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kusimamia misingi iliyoanzisha Bodi hiyo.

Alisema kuwa Wizara ya Fedha itaendendelea kutoa ushirikiano kwa Bodi hiyo ili kuendelea kuimarisha uchumi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Gavaa wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, alisema kuwa Benki Kuu imeendelea kufanya vizuri katika kuimarisha uchumi na hilo linadhihirika baada ya nchi kupitia vipindi tofauti vya msukosuko wa uchumi uliozikumba pia nchi nyingi Duniani.

Post a Comment

0 Comments