NA MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amekagua Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Taaluma na Karakana katika Chuo Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Ndaki ya Rukwa leo 15 Juni, 2025.
Mradi wa ujenzi wa Ndaki ya MUST RUKWA, ulianza mnamo 01 Septemba, 2023 unatarajiwa kukamilika 30 Juni, 2025 unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 11.6 ambapo umefikia asilimia 89 ya hatua za ukamilishaji.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa, Mkandarasi wa Mradi Eng. Peter Laurian amesema Mradi huo ukikamilika utaweza kutoa huduma kwa Wanafunzi zaidi ya 2000 katika ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada kwa Kozi mbalimbali ambao watakuwa msaada mkubwa katika jamii ya sasa yenye Maendeleo Makubwa ya Sayansi na Teknolojia.
Mwenyekiti Kawaida ameipongeza Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini kwa usimamizi wa Mradi utakaochochea kukua kwa Uchumi katika Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini.
Aidha, amewataka Wananchi kuwa mstari wa mbele kulinda miundombinu ya chuo Kwa ukaribu zaidi ili kiwafae Watoto wao na vizazi vijavyo na kwamba, yeyote atakayeharibu hatavumiliwa kwa gharama zote.
Kawaida anaendelea na Ziara yake ya Siku Saba za Kibabe katika Mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe ambayo inatarajiwa kutamatika 17 Juni, 2025.

0 Comments