NA MWANDISHI WETU
Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa amesema kuwa, maendeleo ya Sekta ya Madini yanapelekea kuwa kitovu cha uchumi nchini, hii ni kutokana na mageuzi mbalimbali yanayoendelea kufanyika.
Dkt.Kiruswa ameyasema hayo leo Juni 13, 2025, wakati akizungumza na vyombo vya habari mapema baada ya kutembelea mabanda katika maonesho ya madini yanayoendelea kufanyika wilayani Ruangwa.
Akielezea kuhusu uwekezaji wa ndani Dkt.Kiruswa ameeleza kuwa, Tanzania imekuwa kivutio kikubwa cha wawekezaji katika Sekta ya Madini kutokana na utajiri wake wa madini mbalimbali yakiwemo madini ya kinywe,makaa ya mawe pamoja na madini adimu na madini mkakati.
Kuhusu kukua kwa Sekta ya Madini, Dkt. Kiruswa amebainisha kuwa, Sekta hii imeendelea kukua kwa kasi ambapo kwa sasa inachangia asilimia 10.1 kwenye Pato la Taifa.

0 Comments